Kuna jambo limefanywa na mawaziri hawa kwa nyakati tofati,lakini wote kwa pamoja wanastahili pongezi kubwa sana,binafsi nawapongeza sana na mungu awajalie afya njema,
Msingwa alitimiza wajibu wake kama waziri kivuli kufanya utafiti wa majangili wanaocheza na mbuga zetu kwa kigezo tu eti cha kuwa na kibali cha uwindaji ihali wanakiuka sheria na taratibu za uwindaji,bwana msingwa alionyesha ushahidi wote hadharani na watu tukaona,huu ulikuwa ni uzalendo wa hali ya juu sana ukilinganisha na kariba ya viongozi tulionao tanzania,
Lakini pia waziri nyarandu naye kama waziri mwenye dhamana alifanyia kazi taarifa hiyo na hatimaye kuchukua hatua ambazo zimempendeza yoyote mpenda maendeleo tanzania,kwanza amefuta vibali vya makampuni haya uchwara na pia kuijenga upya sekta hii ya wanyama pori,ambapo sasa imekuwa mamlaka kamili ambayo inatambulika kisheria na wajumbe wa bondi watatokana na wananchi na watakuwa na mamlaka yote ya kusimamaia mamlaka hii kisheria ,,hii ni hatua nzuri na inayofaa kupongezwa.hongera sana ndugu waziri nyarandu,
Pamoja na tofauti kubwa iliyopo baina ya viongozi hawa wa kisiasa lakini wameonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kila mmoja kumpongeza mwenzaka kwa kazi nzuri aliyoifanya,
VIONGOZI WENGINE TUIGE HAYA MFANO WAZIRI WA NISHATI
BW. MSIGWA |
![]() |
BW. NYALANDU |