Sunday, August 3, 2014

VIONGOZI WA SERIKALI YA TANZANIA NI DHAHILI WAMEFUNGWA UFAHAMU NA MUNGU ILI KUSUDI LITIMIE

Habari!
         Ndugu zangu ninayo furaha kubwa sana kuja mbele yenu nikiwa mzima wa siha njema kimwili na kiakili,pia kuwasalimu ndugu zangu wasomaji popote mlipo,mungu awape muda mwingi wa kuishi hapa duniani na abariki ndimi zenu kwa kiasi chake..
       Nipo hapa leo kushirikisha fikra nyingine katika jambo hili ili tufungue mjadala chanya katika sehemu zetu za kazi na sehemu zetu za kupigia songa muda wa mapumziko wa kazi na sehemu zetu za kahawa na kadhalika,jana katika taifa letu kulikuwa na majadiliano pale ubungo katika hotel nzuri yenye hadhi ya kuingia watu wanye mawazo chanya wanaopenda mabadiliko katika dunia hii,yalikuwa majadiliano yaliyoandaliwa na chama cha wanasheria tanzania(tanganyika law sociaty) TLS,juu ya mkwamo wa kitaifa juu ya kupata katiba mpya.,
      Mimi naamini katika imani ya dini fulani ,katika imani yangu mungu amesema hadharani kabisa kwamba ILI



LENGO LAKE LITIMIE HUFANYA YALE YASHANGAZAYO ULIMWENGU,MAKUBWA TUSIYOYAJUA,CCM na viongozi wake hawataki katiba mpya,hawana nia ya kuwaletea watanzania katiba mpya na wapo tayari kwa lolote kuhakikisha katiba haipatikani,mifano iko wazi na iko mingi ya kutosha,lakini niwambie kitu kimoja,ili uamini kwamba mungu anamakusudi mazuri na taifa letu AMEWAFUNGA UFAHAMU HATA HAWAJUI YATAKAYOJIRI MUDA MCHACHE UJAO,kweli hakuna binadamu ajuaye ya baadaye lakini tumepewa utashi wa matokeo ya matendo yetu.lakini kwa ccm na viongozi wake wamefungwa wasipate utashi huu ambao asilimia 99 ya watanzania mungu amewafungulia lakini GETI LIMEFUNGWA KWA CCM,
       Tutashangilia muda si mrefu ushindi mkubwa wa kishindo,maana mungu atawafungulia ufahamu wao asubuhi kumepambazuka huku ukombozi kwa watanzania ukiwa umetamalaki,siombei wakimbie,mungu awape ujasiri wa kubaki ili waone jinsi mungu alivyo mkuu kwa watoto wake baada ya kusikia kilio chao na machozi ya uchungu na damu kwa takribani miaka 50.
        Tunawatia nguvu na maombi makubwa wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili,tutakesha kwa maombi kwa mungu wetu na wao watakesha kwa waganga wao, lakini MUNGU NI MUNGU, ATADHIHILISHA UKUU WAKE MCHANA KWEUPE.Nampa pole kiongozi mkuu wa nchi kwa kuwa naye ameondolewa uhodari wake kwa sababu ya kujihusisha na maovu,mungu hayupo tena naye maana madhambi yao yanahifadhiwa naye,lakini mungu wetu ni mwema anaendelea kukupa neema yake ili taifa letu lipite hapa,si kwa wema na wadilifu wako BALI KUTOKANA NA MAOMBI YA WENYE HAKI WA TAIFA HILI....
   Kila aliye na macho na aone na kila aliye na masikio asikie,tunakumbushana tu uamuzi upo ndani yako,kama unataka tanzania ipone peleka ujumbe mwema kwa nduguyo na rafiki,na kama huamini katika nguvu ya mungu kaa kimya utakutana na nguvu ya mungu mlangoni,,,,,WANAYO MASIKIO LAKINI HAWASIKII, WANAYO MACHO LAKINI HAWAONI,

   barikiwa ndugu