Naomba niwasalimu ndugu zangu wote wasomaji wa blog hii,nilikuwa sipo kidogo kama miezi kadhaa katika uwanja huu wa kupashana habari na kujulishana yale yanayoonekana kwa jicho la makengeza na watawala wetu au wale wenye nafasi katika maamuzi ya maisha yetu,nawasalimu katika jina la mungu wetu aliyer mwema kwa wote,,
Rais wangu ndugu Jakaya yeye ndiyo rais wa taifa hili la tanzania kwa takribani miaka 9 na mwakanai anaende kumaliza muda wake wa kutuongoza,ama ametuongoza vibaya au vizuri pima mwenyewe maisha yako miaka 9 iliyopita yalikuwaje na leo mambo yakoje ,utapata jibu.
Leo kuna jambo dogo tu lakini ni kubwa katika mantiki yake,hili swala la escro ni jambo au ni habari ambaye imeingia kwenye ufahamu wa watu nje na ndani, labda huenda likawa ndilo japo pekee ambalo limeamsha fikra za watanzania kwa miaka 9 yote ya ndugu kikwete na tumeona katika serikali za mitaa,mfano mdogo...haya mambo yanatokea katika nchi ambayo usalama upo,watawala wapo na kila kitu mhimu kipo,swali moja tu je ni nani ambaye anatakiwa kulaumiwa kwa yote haya yanayoendelea,,KAFULILA,ZITTO AU KIKWETE,
Hapa kila mtu ana majibu yake kutokana na uwezo wake wa kufikiri na zaidi analenga masilahi yapi ya kitaifa au masilahi binafsi,yote mungu anayajua,
Ndugu Kafulila yeye ndiye mbuge ambaye alipeleka hoja hii bungeni akiwa na ushahidi na hataimaye watanzania tukajua,bila yeye wewe na mimi tusingejua ila wezi ndo wangeendelea kujua ufisadi wao,,,note,
Ndugu Zitto huyu pamoja na kamati yake ndiye aliye tuletea kwamba hawa wezi waliiba iba vipi na waligawana vipi,pamoja na mapungufu yao lakini taifa limeweza kujua nani aliiba na nani alinufaika na wizi huo na hatimaye wakaja na adhabu zinazowafaa wezi hawa,hungewajua wezi bila zito na kamati yake ,,note
Ndugu Kikwete huyu ndiye anayeshikilia haki na nguvu yetu kama raia wa tanzania,majina ya wezi ameletewa na mapendekezo yake,yeye ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha wezi hawa wanaadhibiwa, lakini akiamua anaweza asiwaadhibu kwa sababu ameamua..then kukawa hakuna cha kumfanya,ila lazima chama chake kitambue kwamba yeye ni taswira ya taifa la tanzania na pia ni taswira ndogo ya chama chake kilichompa ulaji huu,..kuna kila dalili ya watanzania kuchoka na hatimaye wapo tayari kufanya mabadiliko ya kweli kwa njia ya kura na hata kama wakizuia kwa njia ya kura basi ulevi huo wa madaraka utakimaliza chama chao na kuleta machafuko katika taifa .maana watanzania wa leo wnataka mabadiliko ya KWELI.
![]() |
Ndugu; Kafulila--MBUNGE |
![]() |
Ndugu;Jakaya kikwete--RAIS WA TANZANIA |
![]() |
Ndugu; Zitto---MBUNGE |