Wednesday, April 15, 2015
EE MWENYEZI MUNGU TUJALIE KIONGOZI SHUPAVU KAMA HUYU...2015 OCTOBER
Habari,
Tunayo historia kubwa kama taifa,historia ya kutukuka duniani kuwahi kupata kiongozi shupavu mwenye upendo kwa raia wake na aliyeamini katika kukua kwa pamoja kama taifa na pia aliutafsiri uchumi kutokana na maisha ya raia wake na si kutokana na vitabu vya wazungu,.huyu si mwingine ni BABA WA TAIFA LA TANZANIA MWL.JK NYERERE...Upumzike kwa amani.
Tukaja pia tukapata kiongozi wa taifa ambaye kwa mutazamo wake na washauri wake,aliruhusu mtu kufanya chochote,mahala popote,hata wakati mwingine bila hata kufuata taratibu na sheria,ubovu wa mipango miji,watumishi wa umma kushiriki biashara,kuua azimio la arusha,huyu si mwingine ni MZEE WETU ALLY HASSAN MWINYI,,,hapa ndipo msingi wa taifa letu ulianzia kupotea kwa kasi ya ajabu na hili liko wazi kabisa kwamba awamu hii iliitwa awamu ya RUKSA.na huu ulikuwa mtazamo wa ajabu kabisa kupata kutokea duniani kwa kiongozi wa taifa kuruhusu mambo yafanyike kiholela....HATUJACHELEWA...alipata kusema 'kila zama na kitabu chake'
Ikaja awamu ya tatu,ambaye kiongozi wake aliamini katika ubinafsishaji,aliwapa watu mashirika ya umma kwa bei ya kutupwa utadhani hakuna raia ambao wanaweza kuendesha mashirika hayo na hatimaye mashirika yote yaliyobinafsishwa asilimia 70% yamekufa.huu ulikuwa ni mtazamo hasi na usiokuwa na tija kwa taifa,alijitahidi sana mzee huyu kuwa mkali,kwa vyombo vya habari,kwa balaza lake la mawaziri lakini pia alijitahidi kulinda uchumi wetu kwa kiasi fulani,,ingawa naye alifanya biashara ikulu na kuondoa heshima yake mwenyewe japo bado watanzania tunamheshimu sana mzee huyu si mwingine mzee..MZEE BENJAMINI MKAPA kauli yake 'watanzania wana wivu wa kike ' walipojaribu kukemea ufisadi.
Tunaye anayemaliza muda wake wa uongozi wa miaka kumi.mchumi alieshindwa kulinda uchumi wa taifa lake,rais wangu zama zake ni zama za serikali yake kuto kuwa na nidhamu ya kiuongozi,kila mtu anasema,serikali inadondoka kila siku,nchi haina fedha,wezi wachache wanatingisha nchi na serikali yake na yeye bado yupo kimya,,rais ambaye atakumbukwa kwa kufanya safari nyingi za kuomba misaada na hatimaye misaada hiyo haijafika kwa sababu za viongozi wake kuwa wezi wa kupindukia,,tunakutakia kila la kheri katika muda wako wa mapumziko,,huyu ni mzee JAKAYA MRISHO KIKWETE my president,,,kauli yake'akili za kuambiwa changanya na zako' watu waliomzunguka wamemzidi maarifa,
NOTE,,,kila zama za utawala ujinga wetu na upole wetu ndiyo mlango wa kuruhusu watawala hawa kufanya wanayoyafanya,,lazima tujue wajibu wetu kwa taifa letu na pia kudai haki zetu kwa utawala wowowte dhalimu....WHO IS NEXT 2015,,,KAJIANDIKISHE ILI UPIGE KURA NA KUPIGIWA KURA OCTOBER ILI TUKOMBOE TAIFA LETU...usikubali kununuliwa kwa fedha na vijizawadi
Subscribe to:
Posts (Atom)