Thursday, May 14, 2015

KILE KINACHOTOKEA BURUNDI,BILA UMAKINI TUTASHUHUDIA HAPA NYUMBANI

Habari!!!!

       Kile kinachotokea burundi huenda kikatokea na hapa kwetu kwa sababu moja tu kubwa,,,siasa za afrika zinafanana,huenda usinielewe, ila pia unaweza kuamua kutokuelewa kwa sababu tu umeamua.ila ukweli wenyewe ni mchungu sana na pamoja na uchungu wake ni lazima usemwe ili kuliponya taifa letu.
        Kumekuwa na wimbi la ghasia duniani na matukio mbali mbali ambayo kimsingi yanaonesha upande wa pili wa binadamu jinsi alivyo,ubinafsi,chuki,udini na ukanda unazidi kudhihilishwa na wanadamu wa leo kwa matendo yao..mahala popote ambapo haki haipatikani ni shida pia kuona amani ikitamalaki,viongozi wengi wa sasa wa afrika yote wamekuwa wabinafsi wa kupindukia,wanajali ndugu zao na marafiki zao,, na zaidi wanaabudu mataifa tajiri kama miungu yao kwa sababu tu wakubwa hawa watawalinda baada ya kufanya maasi yao katika mataifa yao,na hilo tayari raia hawa walioitwa wajinga leo wameshajua janja yao na wapo tayari kudai haki zao...

  Hapa kwetu tanzania kuna matukio ambayo yanaonesha dalili zote,kwamba kama hakutakuwa na utashi katika maamuzi ya viongozi wetu,basi amani yetu itatoweka haraka sana na tusiipate tena labda katika kizazi cha tatu,,1,vyama vinaruhusu watu kutoa rushwa kupata uongozi 2..raia wemechoka wanapokea rushwa na chochote watakacho ambiwa wanafanya 3..serikali inakusanya kodi kidogo na inatumia kingi katika anasa na si maendeleo 4..serikali haina neno la pamoja,  nchi inaongozwa kwa predication 5..wananchi wamepokwa mamlaka yao ya kikatiba na badala yake viongozi ndo wameshika usukani,,,,
   Naandika leo hii,,kama kutakuwa hakuna utashi ndani ya vichwa vya viongozi wa ccm na serikali yao basi yale yanayoendelea kutokea katika nchi za afrika basi na tanzania ni sehemu ya afrika.nawaombea kwa mungu wetu wasilewe sifa za madaraka nchi yetu ilipofika ni mahala pabaya.kisiasa,kiuchumi,kijamii,kidini,,,na kengere hii iwaamshe katika usingizi wao wa pono wa kufanya vitu kwa mazoea...
   God bless Tanzania,GD BLESS AFRICA