Thursday, August 25, 2016
SERIKALI,JESHI LA POLISI NA CHADEMA RAIA BADO TUNATAKA AMANI YETU,MALIZANENI MAPEMA .
Hii
ni saa ya uzima na ufufuo,ni kauli ambayo hupenda kutumiwa na Askof Gwajima ,huenda isiwe na mantiki kubwa
sana kwako lakini ukiitafakari kwa kina unaweza ona umantiki wa sentensi hii.
Leo taifa letu lipo kwenye mkanganyiko wa
kauli na vitisho visivyo na mantiki katika ustawi wa taifa letu na umoja
wake.ni busara kubwa iliyotumika na waasisi wa taifa hili kuweka katiba
inayopaswa huheshimiwa na raia wote wa Tanzania bila kujali
ukubwa,rangi,kabila,jinsia wala cheo cha raia huyo.
Huo ni utaratibu wa karibu jamii zote za
dunia,wamejiwekea katiba kama mwongozo wa maisha yao na ni dhahiri tumeona
mahala ambapo katiba inaheshimiwa na watu wote amani na maendeleo mahala hapo
hutawala,mifano iko hai,marekani,uingereza na nchi nyingi za ulaya,
Lakini pia kumekuwa na utaratibu wa aina
nyingine wa utawala ambao hauruhusu sana haki za raia kuwa kubwa kuzidi
watawala,tunaona china,korea kusini,cuba,hii ni mifano michache tu.lakini
pamoja na kutoruhusu haki hizo watawala hao wameleta maendeleo ya kweli kwa
raia wao,na hiyo inawapumbaza kwa muda tu,kwa jinsi binadamu alivyoumbwa ipo
siku ataidai haki hiyo ya kusikilizwa ingawaje anapewa kila asali na maziwa na
mtawala wake.atataka kuongozwa siyo kutawaliwa na historia inasema hilo.
Hapa kwetu kuna vitu ambavyo kimsingi
havikufaa hata kujadiliwa na umma wa watanzania ni mambo ambao ilibidi yaamriwe
na viongozi wetu tena kwa kutumia akili ya kawaida tu maana suluhu yake ipo
wazi,
Ila suluhu yake kwa point ambayo tumefika
kama taifa,huenda isiwe suluhu sahihi na itatugharimu wote,watawala na
watawaliwa na kuja kurudisha tena hali ya umoja wa kitaifa it will take time na
huenda vizazi kadhaa hapo mbele vikakutana na matokeo mabaya ambayo viongozi
wetu leo wanashindwa kutatua kwa njia ya amani na udugu.
Polisi na serikali mna wajibika kwa asilimia
kubwa,kuhakikisha amani yetu inaendelea kuwepo,lakini pia opposition kudai haki
kunaendana na wajibu,timizeni wajibu na serikali itoe haki kwa raia wake kwa
mjibu wa sheria na asasi zote ambazo zipo kisheria zitimize wajibu wake kwa
mujibu wa taratibu na sheria zetu.
Polisi mnao wajibu wa kulinda raia na mali
zao bila kuwa na itikadi ya kuwagawa raia hawa,mkitimiza wajibu huo TANZANIA
itakuwa na AMANI,ila kwa m
ienendo ya siku za hivi karibuni huenda kukawa na sehemu
mmejikwa kidogo,rekebisheni raia bado wanawaheshimu,lakini niwape pole jeshi la
polisi kwa askari wetu waliouwawa na majambazi,hili si jambo jema na lazima raia tushiriki
kuhakikisha majambazi haya yanakamatwa na sheria ichukue mkondo wake.
![]() |
Askari wakiwa mazoezini |
UJUMBE KUTOKA KWA RAIA WA KAWAIDA TU.
Subscribe to:
Posts (Atom)