Karibu,
Kitendo chochote ambacho binadamu anafanya kina mwanzo na mwisho wake, kama vile biblia inavosema juu ya hili, kwamba kila jambo na wakati wake,wakati wa shida na wakati wa raha, wakati wa kucheka na wakati wa kulia, hii ni mifano tu kati ya aina nyingi za nyakati.
Sasa leo nataka ndugu zangu tuone umuhimu au unyeti wa sentensi hii MARA MOJA (ONETIME)katika uwanda mzima wa mahusiano.
Mara nyingi maisha yetu yanabebwa kwa asilimia kubwa na mawazo yetu, yanayopelekea maamuzi yetu, na hayo maamuzi yetu ndo hupelekea kitu kinachoitwa maisha kuwa kina maana... maana namna unavofikiri na kutenda ndo tafsiri ya maisha hapa duniani.
Kuamua kutongoza mtu ambaye unadhani unampenda hutokea mara moja,na kukubaliana kwa matakwa hayo baina ya nyie wawil hutokea mara moja.lakini pia kufanya ngono huanza mara moja.... na hapo sasa ndo umuhimu wa sentensi hii inaanza kuonekana.....
Matokeo chanya au hasi hutokea baada ya ngono ya mara moja,labda mimba au magonjwa baada ya tendo la mara moja.
Mara moja hii kama utaitumia vibaya bila kutafakari kwa kina basi unaweza kupoteza maisha yako au kuingia kwenye mateso ya mda mrefu kutokana na kitu mara moja tuuuuu......
Kama unataka au una ndoto ya kuwa mtu chanya kwa mataifa, basi jiepushe sana na hii kitu,mara moja tu
.Afrika ni moja kati ya bara linaloongoza kwa magonjwa yatokanayo na maambukizi ya ngono ikiwepo ukimwi na magonjwa mengine mengi ,kama saratani ya shingo ya uzazi na mengine mengi.....
Kama imetokea kwa ndugu yako au jamaa yako, jirani yako, huu ni muda wa kutumia hii sentensi katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii yako inayokuzunguka..........
NGONO ZEMBE INAUA MAMILIONI YA WATU DUNIANI ,ONETIME MLINDE JIRANI NA RAFIKI YAKO,,,,,,,,,ONETIME
No comments:
Post a Comment