Jana ndugu rais aliongea na wazee wa dar es salaam,ikiwa ni ujumbe kwa taifa zima,hotuba ile inajenga utaifa na tanzania kuwa taifa la kujitegemea katika picha yake,lakini juhudi hizi la rais pamoja na baadhi ya watendaji wake hazitazaa matunda kama raia wenyewe hatutakuwa sehemu ya mabadiliko haya au mageuzi haya.
Tutashiriki kwa kufichua waharifu walipo,lakini pia kwa kulipa kodi, zaidi kudai risiti halali ya tra katika manunuzi yetu,hili pekee litasaidia kupiga hatua za haraka katika maendeleo tunayoyataka,lakini pia kuwe na uelewa juu ya nini hasa maana ya maendeleo,kwa viongozi wetu na raia wenyewe.huwezi kuwa na maendeleo endelevu katika taifa kama hutaweka mifumo imara katika idara zote za serikali, mifumo imara huzalisha watu makini,lakini mara nyingi watu makini huwa hawaamini katika mifumo na huona wao binafsi kama ndiyo majibu sahihi ya matatizo fulani ya raia,ni kweli kwa upande mmoja lakini wanasahau kwamba wao pia ni binadamu tu kama wengine wenye haki sawa na wengine mbele za mungu,.
Vinginevyo namtakia kila jambo la kheri mr rais pombe achape kazi twende mbele,vija
![]() |
Mr President Pombe John Magufuli |