Friday, February 12, 2016

SIKU 100 ZA RAIS MAGUFULI IKULU

  Habari,
     Napenda kutumia fulsa hii adimu kueleza kile kilichojitokeza katika siku 100 za mheshimiwa rais john pombe ikulu,kuna mambo mengi ameyafanya kama rais na pia baada ya kuunda serikali yake yapo yaliyofanywa na wasaidizi wake mazuri na mabaya,
   Mazuri ambayo yanaonekana kwa macho yetu ya nyama ni kwamba amepunguza safari zisizo na tija,hafla zisizo na maana japo hapo napo ipo shaka,lakini pia ameweza kuonesha ishara ya watu kuwa na nidhamu na kazi zao,ukiyachukua haya yote unaona dhamiri chanya ndani yake juu ya taifa letu,ni jambo jema na ni jambo la kujivunia.
   Mabaya yake ambayo nilazima yasemwe ili wajue na wafanyie kazi,kuminya uhuru wa bunge na kupanga kamati mhimu kimkakati,mbili kusitisha matangazo ya tbc live na kurusha edited si dalili njema kwa utawala bora,pia kutokuweka msingi wa maono yake katika katiba ya warioba bado ni tatizo lisilo na mfano,maana president pombe yeye ni binadamu anaweza kuchukuliwa na mungu muda wowote,kwa hiyo kumpata mtu kama yeye si rahisi sana japo inawezekana.kwa hiyo tunahitaji mambo yote yawekwe katika sheria mama(katiba)
   Lakini pia amezuia bunge kurushwa live lakini katika sherehe za hovyo tu za chama wanarusha live,je chama kina fedha kuliko serikali?ama chama ni mali ya uma?ama ni ubabe wa kimadaraka au kutokuwa na ufahamu juu ya utawala wa sheria?
Nyarugusu refugee camp-Tanzania
  All in all namtakia kila lililo la kheri,afanye kazi kwa bidii akumbuke katiba ndiyo msingi wa nchi kutulia na kuwa na uchumi imara,na zaidi akumbuke zanzibar ni sehemu ya jamhuri kama hakuna political stability upande mmoja wa muungano basi taifa zima litakosa utulivu,"hakuna uvunjwaji wa sheria usio na chanzo duniani,na chanzo kikuu cha uvunjwaji wa sheria ni pale serikali ikiacha kutimiza wajibu wake"

No comments:

Post a Comment