Saturday, October 15, 2016

matendo siku zote hayana nyongeza

  Salam!
       napenda kutumia fursa hii kusema na ndugu zangu jambo moja mhimu sana ambalo litatusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweka ubora halisi wa maisha yetu,
    Kila binadamu hutenda jambo,lakini kabla ya kutenda huaza kwa kina au huwaza kawaida na hatimaye hutenda.leo nataka mtu ajue kwamba ukitaka kutenda jambo fikiri mara mbili maana katika matendo hakuna nyongeza ya tendo,ukitenda subiri matokeo yake no way out.
  Na matokeo haya yanaweza kuwa matokeo chanya au matokeo hasi,maana maisha hayana majaribio vile ulivyoamua leo ndiyo maisha yenyewe,so chunga sana mawazo yako ambayo ndiyo yatakupelekea utende.

Monday, October 3, 2016

SEMA NAWEZA NA UTAWEZA


Rais anayetaka kuua raia wake zaidi ya milion tatu ni huyu hapa

Salam ndugu zangu,
      Katka maisha yetu ya kila siku lazima tuwe na utaratibu wa kujifunza mambo yanayoendelea dunia,leo hii kuna raisi wa taifa ambalo lipo hapa duniani anachukizwa na hali iiyopo katika taifa lake na kufikia hatua ya kutaka kuua watu milion tatu,tena anatamka hadharani.
     Na sio anataka tu kuua lakini tayari ameshaua watu zaidi ya elfu tatu mia tano,watu wanaojihusisha na madawa ya kulenya na watumiaji,hii ni hatari kwa uhai na haki za binadamu duniani,japo hali yenyewe ya matumizi ya madawa ya kulevya haikubaliki pote duniani lakini kwa adhabu hii,ni kubwa kuliko.
     Huyu ni rais mpya kabisa wa taifa la philipines ambalo lina idadi kubwa ya wakristo duniani,hana mwaka mmoja madarakani lakini hataki mchezo kabisa,anaitwa HON.RODRIGO DUTERTE,lakini je mbinu ya kutokomeza madawa ya kulevya ni kuua?
     Hapa duniani kuna tasisi nyingi sana ambazo zinaingiza fedha nyingi kutokana na bishara hii haramu na si katika nchi ndogo la bali kwa hawa hawa akina bwana mkubwa,ulaya,amerika zote na hata hapa kwetu afrika,jambo pekee ambalo litaleta unafuu katika vita hii ni kutoa elimu ya kutosha kwa raia juu ya madhara yake ili wakosekane watumiaji na hatimaye biashara hii itakoma.
    Lakini kama vyombo vya habari vinatoa airtime kubwa kwa kampeni za madawa ya kulevya na kusema thamani ya madawa hayo live,hii inawavutia vijana kuona hiyo kama fursa ya kuingiza fedha,and are going there to make it happen.lazima kuwa na kampeni ya pamoja tena kampeni chanya.
    Kuua mtu kwa sababu yoyote ni kosa,lakini pia mtu mlaibu wa madawa ya kulevya muda wake wa kuishi ni mchache mno,so hata ukiamua kumua unakuwa umepata dhambi mbaya tu tena ya bure,maana hata ungemwacha angejifia mwenyewe,
    Dunia haitaki kuona hilo linatekelezeka na huyu raisi yeye ameiambia dunia yuko tayari kujitoa katika jumhiya ya umoja wa mataifa ili adhima yake aitimize ya kuua watu milion tatu watumiao madawa ya kulevya nchini philipiness.
    Watanzania  tupo?kazi kwetu tujitafakari pia nasi nyendo zetu tufanye kazi kwa bidii bila kupenda njia za mkato,