Monday, November 14, 2016

KWA NINI TRUMP NI MHIMU KWA DUNIA YA LEO?

 Napenda kutumia fursa hii kusema hili ambalo hasa lipo moyoni mwangu na akili yangu inaniambia hivyo,
  Waafrika wengi ambao tunatoka afrika tuliopo mahala pote pa dunia  hatupendi kuambiwa ukweli,na mr Trump anasema ukweli,amabao sisi hatuutaki.
  Leo katika Tanzania yetu tunaye president ambaye anahimiza watu wafanye kazi waache kulalamika na wafanye kazi kwa didii zao zote na kwa uadilifu,lakini bado anaonekana hafai,mara hela hazipo,mara nduvu ya soda mara nini,hii yote ni dalili mbaya sana kwa mwanadamu hupaswi kulala
mika inapaswa uchukue hatua ya kutatua tatizo.
   Bwana trump amejipambanua tangu kipindi chake cha kampeni kwamba,atasema ukweli japo utawauma watu lakini ni ukweli na ndiyo jibu sahihi la matatizo Fulani yaliyopo duniani.
  Mosi..,swala la wahamiaji haramu,hajakataza watu kuingia amerika kasikazini(marekani)bali anataka watu waingie kwa kufuata utaratibu uliopo,na ndiyo dunia nzima inafanya,kama unataka kwenda nyumbani kwa mtu lazima ufuate utaratibu wake ambao mara nyingi ni wa kawaida tu kama shabaha yako ya kufika mahala hapo ni chanya.
   Mbili…ugaidi na uisilam,watu hawajaelewa hasa nini mantinki yake,middle east yote leo inapigana na imesambaratika kweli na wanaopigana ni wenyewe kwa wenyewe,na huko kote asilimia 95% ya raia wao ni waislam ama shia ama suni.vikundi vyote vinavyoendesha mauaji ya kutisha hapo middle east ni muslim,amabo wanaitumia vibaya dini ya mtume,lakini mahala wanapojificha ni kwenye mwavuli wa uislam,ndio maana trump anasema,amerika imeshishiriki katika vita nyingi huko middle east,na wakimbizi wanapokuja ulaya na marekani kwa wingi,bado wanahasira na marekani,kama bado wana hasira na marekani anytime wanaweza kulipa kisasi,kama tulivyoona katika milipuko mingi ya kujitoa mhanga marekani na ulaya wanaohusika ni watu wenye asili ya middle east,na wanaoamini katika uislam japo si waislam halisi,anasema amani itafutwe kwao,misaada iende kwao ili waelewane kwanza wenyewe na wale wanaotaka kwenda marekani waende kwa sababu za msingi,ukitazama kwa jicho la kawaida huwezi kuona mantiki ya hili.
  Tatu…Afrika kwanini watu wake ni masikini na wanakimbilia marekani na kufanya uwekezaji kule badala ya kuja kwao wawekeze?kwa mtazamo wangu hata kesho wangerudishwa wote,waje tulijenge bara letu,maana hayupo mtu atajenga bara letu kama wenyewe  tunakimbia,na ni jambo jepesi tu kuelewa kwamba katika zama hizi za maendeleo makubwa ya dunia,kuwa na nchi ambayo inategemea misaada kwa zaidi ya asilimia 50% ni aibu,tena aibu sana.tumuunge mkono rais yoyote anayehimiza watu wafanye kazi,wawe waadilifu,wawe na uzalendo na mataifa yao.

    Mwisho msiye mtaka kaja,presidenti pombe bahati nzuri ameanza kutuzoesha kuisha maisha halisi siyo ubabaishaji kama awali,fanya kazi ndiyo ule tena kazi halali,na Bwana mkubwa trump kuanzia January 2017 misaada mingi sana itakoma na atafanya yale anayoona yana masilahi kwa marekani..so tufunge mkanda wa kujiandaa kupokea mabadiliko makubwa ya kiuchumi duniani.

No comments:

Post a Comment