Monday, September 30, 2013

DHANA YA VIJANA KUWA NA MPENZI ZAIDI YA MMOJA ,JE UPO KATIKA VIJANA WENYE TABIA HIZI;

Salamu,,,
 Kwanza kabisa niwasalimu vijana na wazee wangu, salamu itokayo kwa kristo yesu mfariji wetu, barikiweni na neema ya bwana itamalaki njia zenu na maisha yenu ya kila siku.( emeni.)

 Kuna vijana na watu wazima,waliompokea yesu na wasio mpokea yesu wenye tabia za kuwa na mahusiano ya kingono na mpenzi zaidi ya mmoja.hatari iliyopo hapo na upendo uliopo hapo ndio unatusukuma na kuona hii ni njia sahihi kabisa ya sisi kama jamii kulijadili kwa namna ya upana wake na ushirikishi wa kutosha kwa watu wote bila kujali imani zetu.
      Ukijiona unawaza na kuamua kutokana na sentensi mojawapo kati ya hizi,basi utapata jibu lake mwisho kabisa,nakusihi soma mpaka mwisho;

1--Unampenda mtu kwa sababu ya uchumi wake,

2--Unalipiza kisasi kwa sababu muda mwingi uliutumia shule au geti kali,

3--Unawaridhisha   marafiki zako ili wakuone wewe ni noma kwelii kwa ngono, unadhani ukiacha watakucheka,
4--Unafanya ngono kama dozi ya panadol asubuhi , mchana, jioni,unadai eti we ni mkaliii

5--Unajifunza mitindo ya ngono katika intanet na  video mbali mbali...eti ujuzi!

6--Kinachoona mpenzi ni jicho na jicho ndo linakwambia limependa na wewe unapeleka mwili wako,

7--Huamini kama unaweza kuachwa muda wowote na mpenzi wako kwa sababu zozote zile,

8--Huwezi kusamehe na kusahau, wewe katika maisha yako kisasi kipo machoni na mkononi

9--Kusema ukweli kwako ni mpaka kwa dakitari, maana pale lazima  useme kinachokusumbua ili upate tiba sahihi au njaa ikiuma
10---Kila jambo lako la mahusiano linaushauri kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki,liwe baya au zuli.

Hizo hapo juu ni baadhi ya tabia za watu tunayeishi hapa duniani,kila mmoja wetu akisoma hapo juu basi atapata hata japo tabia moja kati za hizo.
 Angalizo, watu wote tunaowaona wanapata taabu na shida ambazo siyo rahisi kuelezeka kutokana na matatizo ya mahusiano,walikuwa na tabia kama hizo hapo juu na wengine bado zimewaganda shingoni mwao na wanatembea nazo kila siku,
     Hakuna mtu ambaye atayajua  mateso na maumivu utakayo yapata kutokana na maamuzi yako.jifunze kwa jirani yako ,ndugu, jamaa  ama rafiki maana magonjwa ni mengi na yanazidi kuangamiza watoto wa mungu walioumbwa kwa mfano wake.
     Yapende maisha yako, yapende maisha ya jirani yako maana adui wa maisha yako ni wewe mwenyewe.jihoji ndani ya moyo wako na uchukue hatua haraka maana kesho siyo siku yako,ukichelewa leo na kesho hutawahi..

HONGERA KWA KUSOMA UJUMBE HUU CHUKUA HATUA SASA

Saturday, September 28, 2013

WASILIANA NA HUYU NDUGU ILI VIDEO YAKO YA NYIMBO ZA INJILI IPATE KUINGIZWA NA KUTAMBULISHWA KWA  WADAU MBALI MBALI KARIBUNI------ BY ADMIN WA  www,httt/itikanasi .blogspot.com
 Ukikaribishwa jambo jema basi lazima nawe akaribie ,maana jukumu la kupeleka injili ya bwanawetu yesu kristo ni ya kila aliye na mwili , hasa wale ambao tayari wameijua kweli na hiyo kweli inawaweka huru na minyororo ya shetani.

KWANINI VIJANA WENGI SIKU ZA LEO HAWATAKI KUOA?

NDUGU, HAMZA MKWILA NA MKEWE WAKIWA KATIKA NYUSO ZA FURAHA BAADA YA KUFUNGA PINGU ZAO ZA MAISHA  HAPA JIJINI DAR ES SALAAM

Kama unadhani maisha ni jinsi unavyoona wengine wanaishi basi na wewe ishi maisha yako  ili wengine waone kwako.kwa kuwa maisha siyo maagizo basi uziigize pia-----kwa vijana wote

NDOANO YETU -BWANA ANATUPENDA TUKAE KATIKA PENDO LAKE

                Psalm 33;16-22
But the eyes of 
the LORD are on to those
 who fear him,

on those whose hope is in
  his unfailing
 love

ONE TIME UMUHIMU WA SENTENSI HII KATIKA MAHUSIANO

Karibu,
         Kitendo chochote ambacho binadamu anafanya kina  mwanzo na mwisho wake, kama vile biblia inavosema juu ya hili, kwamba kila jambo na wakati wake,wakati wa shida na wakati wa raha, wakati wa kucheka na wakati wa kulia, hii ni mifano tu kati ya aina nyingi za nyakati.
        Sasa leo nataka ndugu zangu tuone umuhimu au unyeti wa sentensi hii MARA MOJA (ONETIME)katika uwanda mzima wa mahusiano.
       Mara nyingi maisha yetu yanabebwa  kwa asilimia kubwa na mawazo yetu, yanayopelekea maamuzi yetu, na hayo maamuzi yetu ndo hupelekea kitu kinachoitwa maisha kuwa kina maana... maana namna unavofikiri na kutenda ndo tafsiri ya maisha hapa duniani.
       Kuamua kutongoza mtu ambaye unadhani unampenda hutokea mara moja,na kukubaliana kwa matakwa hayo baina ya nyie wawil hutokea mara moja.lakini pia kufanya ngono huanza mara moja.... na hapo sasa ndo umuhimu wa sentensi hii inaanza kuonekana.....
        Matokeo chanya au hasi hutokea baada ya ngono ya mara moja,labda mimba au magonjwa baada ya tendo la mara moja.
        Mara moja hii kama utaitumia vibaya bila kutafakari kwa kina basi unaweza kupoteza maisha yako au kuingia kwenye mateso ya mda mrefu kutokana na kitu mara moja tuuuuu......
        Kama unataka au una ndoto ya kuwa mtu chanya kwa mataifa, basi jiepushe sana na hii kitu,mara moja tu
.Afrika  ni moja  kati ya bara linaloongoza kwa magonjwa yatokanayo na maambukizi ya ngono ikiwepo ukimwi na magonjwa mengine mengi ,kama saratani ya shingo ya uzazi na mengine mengi.....
       Kama imetokea kwa ndugu yako au jamaa yako, jirani yako, huu ni muda wa kutumia hii sentensi katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii yako inayokuzunguka..........
         NGONO ZEMBE INAUA MAMILIONI YA WATU DUNIANI ,ONETIME MLINDE JIRANI NA RAFIKI YAKO,,,,,,,,,ONETIME
       

Monday, September 23, 2013