Salamu,,,
Kwanza kabisa niwasalimu vijana na wazee wangu, salamu itokayo kwa kristo yesu mfariji wetu, barikiweni na neema ya bwana itamalaki njia zenu na maisha yenu ya kila siku.( emeni.)
Kuna vijana na watu wazima,waliompokea yesu na wasio mpokea yesu wenye tabia za kuwa na mahusiano ya kingono na mpenzi zaidi ya mmoja.hatari iliyopo hapo na upendo uliopo hapo ndio unatusukuma na kuona hii ni njia sahihi kabisa ya sisi kama jamii kulijadili kwa namna ya upana wake na ushirikishi wa kutosha kwa watu wote bila kujali imani zetu.
Ukijiona unawaza na kuamua kutokana na sentensi mojawapo kati ya hizi,basi utapata jibu lake mwisho kabisa,nakusihi soma mpaka mwisho;
1--Unampenda mtu kwa sababu ya uchumi wake,
2--Unalipiza kisasi kwa sababu muda mwingi uliutumia shule au geti kali,
3--Unawaridhisha marafiki zako ili wakuone wewe ni noma kwelii kwa ngono, unadhani ukiacha watakucheka,
4--Unafanya ngono kama dozi ya panadol asubuhi , mchana, jioni,unadai eti we ni mkaliii
5--Unajifunza mitindo ya ngono katika intanet na video mbali mbali...eti ujuzi!
6--Kinachoona mpenzi ni jicho na jicho ndo linakwambia limependa na wewe unapeleka mwili wako,
7--Huamini kama unaweza kuachwa muda wowote na mpenzi wako kwa sababu zozote zile,
8--Huwezi kusamehe na kusahau, wewe katika maisha yako kisasi kipo machoni na mkononi
9--Kusema ukweli kwako ni mpaka kwa dakitari, maana pale lazima useme kinachokusumbua ili upate tiba sahihi au njaa ikiuma
10---Kila jambo lako la mahusiano linaushauri kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki,liwe baya au zuli.
Hizo hapo juu ni baadhi ya tabia za watu tunayeishi hapa duniani,kila mmoja wetu akisoma hapo juu basi atapata hata japo tabia moja kati za hizo.
Angalizo, watu wote tunaowaona wanapata taabu na shida ambazo siyo rahisi kuelezeka kutokana na matatizo ya mahusiano,walikuwa na tabia kama hizo hapo juu na wengine bado zimewaganda shingoni mwao na wanatembea nazo kila siku,
Hakuna mtu ambaye atayajua mateso na maumivu utakayo yapata kutokana na maamuzi yako.jifunze kwa jirani yako ,ndugu, jamaa ama rafiki maana magonjwa ni mengi na yanazidi kuangamiza watoto wa mungu walioumbwa kwa mfano wake.
Yapende maisha yako, yapende maisha ya jirani yako maana adui wa maisha yako ni wewe mwenyewe.jihoji ndani ya moyo wako na uchukue hatua haraka maana kesho siyo siku yako,ukichelewa leo na kesho hutawahi..
HONGERA KWA KUSOMA UJUMBE HUU CHUKUA HATUA SASA
No comments:
Post a Comment