Hapana shaka katika hili ndugu zanguni,habari zenu za ujenzi wa dunia hii tuipitayo,.
Leo nataka tujue au tujufunze kitu kidogo tuu ila chenye maana kubwa sana katika maisha ya binadamu hapa duniani na maisha baada ya kifo.
Vile ambavyo tunaishi leo ndiyo hivyo tunavyotengeneza maisha yetu ya kesho ama tukiwa hai au tukiwa katika hali ya namna nyingine si jinsi ya miili hii tuliyonayo.
Katika maisha ya kawaida tunadhani kwamba sisi twajua kila kitu lakini kwa bahati nzuri mungu wetu ni yeye asiyechunguzika mwisho wa kufikiri kwetu mwanzo wa wake wa hekima,napenda sana kuawmbia ndugu zangu ukishindwa kutambua kwa kamilifu kwamba yapo maisha mengine baada ya kifo basi utapata shida sana hata kutambua baadaye yako.
Maamuzi ya mtu ndiyo hupima kwamba ni kwa kiasi gani anafahamu asili yake na asili ya maisha ya mwanadamu hapa duniani.
Ili kuwa na kesho yenye matumaini lazima umuishie kristo yesu, umkaribishe katika moyo wako na aishi ndani yako siku zote za maisha yako. kinyume na hapo utapotea ndio maana mwimbaji mmoja wa nyimbo za injili aliimba wimbo mmoja usemao PEKEE YANGU SIWEZI.
Pekee yako huwezi kumshinda mfalme wa anga ibilisi shetani,ambaye kila sekunde ya pumzi yako anataka uwe mufuasi wake ili shimo la moto liambatane nanyi wakati wa hukumu ya haki...
MTETEZI WETU YUU HAI tutende yale aliyoyaamuru bwana wetu yesu kristo ili tukavishwe taji zetu baada ya kazi tuliyotumwa duniani kutimiliza BARIKIWENIJ
No comments:
Post a Comment