Kundra za mwenzi mungu zinahitajika,,,,
Kwanza kabisa napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha watanzania kwamba kila kitu katika nchi yetu kipo ili watu waendelee kuishi,nashawishika kuamini kwamba bara zima la Afrika ni lazima tufanye mabadiliko makubwa sana katika sekta hii ya kisiasa.
Siasa imekuwa mwiba wa uchungu sana kwa maendeleo ya wana wa afrika,kwa maana gani?kila nchi ya hapa Barani Afrika imepata matatizo ya yatokanayo na siasa, katika siku za za hivi karibuni nchi yangu ya tanzania imeingia katika mchakato wa kupata KATIBA MPYA YA NCHI.
Ipo nia ya dhati kabisa kwa baadhi ya viongozi wa siasa na wapo pia ambao nia hiyo haionekani katika mioyo yao bali inaonekana katika macho yao.unapata wakati mugumu sana kuelewa,,Nani ni nani katika nchi hii,yupi anamaamuzi yapi,kauli ipi ndo kauli ya mwisho,maana sasaivi kila mtu anasema, tena maneno mazito ambayo ukiyatafakari sana, unaona kama angekuwa mtoto tungesema huyu mtoto amedekezwa na wazazi au walezi wake.,maana mheshimiwa RAIS ambaye ndiye amiri jeshi mkuu wa nchi hii yupo na yupo kimya,japo kimya kingi kinashindo mkubwa lakini kwa Afrika yangu bado ni kitendawili kikubwa ambacho labda huunda kikaja kuteguliwa na kizazi cha mabadiliko ambacho bado sijakiona kwa macho ya ndani ila katika macho ya nyama kizazi hiki kipo.
Kuna muungano wa vyama vya siasa hapa na baadhi ya asasi ambazo zimetoka wazi wazi kupinga muswada uliopitishwa na BUNGE( JMT)pale dodoma.waliopitisha ni wabunge na wanayohaki ya kufanya kile walichokifanya,hiyo itabaki kuwa hivyo.
Hakuna hoja ambayo itakuwa hoja ya maana sana kuliko hoja nyingine,kama watu wachache wanaweza kuchukua haki ya mtu ya msingi ambayo amezaliwa nayo na kufanya hiyo haki imezwe na itikadi ya kundi fulani.kwa hiyo hapo hoja hiyo, itakuwa haina maana yoyote ile kwa mtu huyu.
Jaji warioba na timu yako mmefanya ya kwenu,mazuri na yameonekana kwa macho,haya yote yanayotokea ni kutokana na uhalisia mliouweka katika rasimu hii ya kwanza ya katiba,endeleeni kuwa na hekima na siku ya kufanya maamuzi magumu basi fanyeni maamuzi yenye hekima na busara ili kumbu kumbu yenu ibaki katika vizazi na vizazi,,
MH RAIS, Miaka kumi ya ikulu ni miaka mingi sana katika kuweka historia, Histori kwa kawaida zipo za aina mbili tu,historia mbaya na historia nzuri ya kukumbukwa na kuigwa na vizazi. kwa umri wako mh rais kiongozi wako mkubwa na wa kwanza tena mtetezi wako ni HEKIMA NA BUSARA maana hutoka kwa mungu.tazama kwa makini na uamue kwa makini maana amani ya nchi hii ipo mikononi mwako..itikadi zetu zitapita ila nchi na ardhi ya tanzania itabaki daima.
Kama kuna jambo raisi duniani basi ni kuwa na upendo kwa jamii inayokuzunguka ila ni nadra sana kwa watawala wa dunia hii kuona hilo,,,MUNGU IBARIKI TANZANIA ,WABARIKI VIONGOZI WAKE UWAPE HEKIMA YA MAAMUZI...
No comments:
Post a Comment