Wednesday, October 23, 2013

TIBA MUBADALA KURUHUSIWA KUTUMIKA KATIKA HOSPITALI ZA SERIKALI

Hallow;;
   Katika hali isiyo kuwa ya kawaida mheshimiwa waziri mwenye dhamana ya afya BWANA MWINYI.amewatangazia watanzania kwamba muda si mrefu tutaanza kushudia tiba mubadala katika hospitali zetu za serikali..
     Sio jambo baya ni jambo zuri tena zuri sana.ila kuna mambo kadha ambayo mimi najiuliza na ningependa pia wanajamii tuungane pamoja kuuliza haya maswali kwa ndugu waziri..
  1--Je hawa waganga wa jadi au tiba mbadala watakuwa chini ya idara ipi itakayo waasesi.

2---Vigezo vya hawa waganga itakuwa ni jambo la wazi au ni siri kama ilivyo kawaida.

3---Serikali haina majengo je hawa waganga watakaa katika majengo yapi?

4---Serikali imejiandaa vya  kutosha kuruhusu hili jambo?

5---Kuna waaguzi na watoa tiba ambao wamerithishwa hizo huduma na babu au bibi zao.je mh Mwinyi ameliona hilo kwa jicho la karibu.

6---Maabara za kupimia hizo dawa zao zimeandaliwa na pia bajeti mwaka huu wa fedha itaongezeka kwenye wizara husika?
        Ninayo imani kubwa kwamba China ni moja kati ya nchi kubwa kiuchumi duniani,yenye idadi kubwa ya watu na pia yenye watalaam mbali mbali waliobobea katika fani hizo.....tumeiga huko. je itatusaidia kwa haraka......tujipe muda wa kufikiri kwa umakini...

No comments:

Post a Comment