Leo imekuwa siku ya huzuni sana kwa ndugu hawa wawili ambapo rufaa yao imekataliwa rasmi na kwa tafsiri hiyo hawa ndugu watatumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela,
Baba na mwanae ambao walikuwa rumande tangu 2004 mpaka leo ambapo msumari wa mwisho umepigiliwa katika maisha yao na kuwaachia maumivu ya kutosha kutoa machozi machano pao,hakuna sababu ya kuwa na huzuni sana maana kila kitu katika dunia hii kinatokea kwa muda na kwa sababu maalumu.
Siku sababu hiyo ikitoweka basi na jambo hilo hutoweka pia, napenda kuwapa moyo ndugu na jamaa wa ndugu hawa ili wawe na moyo wa upendo na uvumilivu,wazidishe maombi ili mungu awaoneshe mambo makubwa na ya ajabu ambayo yalikuwa yamefichwa na yanaendelea kufichwa katika macho yetu haya ya nyama....
KILA KITU KIPO KWA MUDA NA KWA SABABU JUU MBINGUNI NA HAPA ARIDHINI
![]() |
Add caption |
No comments:
Post a Comment