Saturday, November 30, 2013

NI UZALENDO UPI AMBAO VIONGOZI WANATUONENSHA WATANZANIA KUZIONA FURSA?

Salama wanajopo natumai mu wazima wa siha njema.

Kwanza kabisa napenda nimpongeze rais wangu jakaya kwa jambo moja la msingi ambalo amelifanya hivi majuzi,kuhudhulia  na kutoa hotuba katika semina ya fulsa hapa dar es salaam.

Mimi ninayo maoni yangu ambayo siyo tofauti sana na jakaya na wazungumzaji wengine katika semina ile.bali kuna jambo ambalo liliachwa kusemwa kwa makusudi au walitindikiwa na mambo mengi  kutokana na  kile wanachokiita ujenzi wa taifa.

MOJA-Serkali imeshindwa kutekeleza dhana ya kilimo kwanza kwa vitendo hii iko wazi,je mtu mmoja mmoja ataweza kumudu suala ambalo watu wenye kila aina ya rasilimali wameshindwa?

MBILI-Hakuna mkulima mdogo ambaye anaweza kulima kwa tija kwa kutegemea jembe la mkono na neema za mwenyezi mungu alete mvua.

TATU-Pamoja na kwamba hicho kidogo ambacho wanakipata kwa kutumia jembe la mkono,bado serikali ndo inawapangia bei,hii si haki na lazima jambo hili jakaya ulione kwa jicho pevu.

NNE-Sera ya ardhi na mikopo tanzania si rafiki na huyu mkulima mdogo ambaye mnamwonyesha fursa.
NB---Nini kifanyike,kwanza kabisa rekebisheni sera ya ardhi na sera ya mikopo katika tasisi za fedha riba ni kubwa mno ili vijana waweze kuzitumia hizo fulsa vilivyo.

No comments:

Post a Comment