Habari zenu ndugu zanguni,,
Nashukuru sana mwenyezi mungu kwa kunipa uwezo wa kuiona leo na akanipa pia wasaa wa kuandika taarifa hii kwa ufupi sana,bunge letu la tanzania limezidi kuwa na vituko lakini kwa kituko hiki, hapana lazima tuweke sawa.
Kuna mbunge mmoja anaitwa mr nchemba pale bungeni kamwambia mwenzake mr mbowe kwamba anatumia madaraka vibaya na kimada ambaye pia ni mbuge wa viti maaluma chadema.sina tatizo na taarifa yake wala siyo jambo zuri kuwa na kitu alafu unakisema kwa mafumbo mafumbo huo huitwa unafiki,kwa hiyo kwa hilo bwana mwigulu, mimi binafsi nakupongeza kwa kuacha kuwa mnafiki.
Ila shaka yangu ni kwamba kama siasa yetu imefika hapa basi hatapona mtu maana asilimia kubwa ya wakubwa wetu hawa wanaongoza kuwa na nyumba ndogo au vimada,kwa hiyo mtu yeyote ambaye anataka kulisema hili lazima kwanza ajihoji mwenyewe usafi wake ndipo aende kwa jirani yake.
Lakini pia kuacha kujadili mambo ya msingi yanalolihusu taifa na kujadili mtu na maisha yake hili nalo ni upungufu kwa siasa zetu za tanzania maana tangu ngazi ya juu tungesema mwenyezi mungu aweke wazi yale yanayotendeka ,basi hata angepatikana kiongozi mmoja au wawili tu waadilifu na ndoa zao..KWA KIFUPI HAKUNA MWENYE UBAVU WA KUMSEMA MWENZIE KWA TABIA ZAO HILI NI JAMBO AMBALO LAZIMA MJIREKEBISHE;;;;
No comments:
Post a Comment