Sunday, January 12, 2014

BIBI WA ZAIDI YA MIAKA 50 ATARAJIA KUPATA MTOTO WA DILI A.K.A MJUKUU WAKE

Katika hali ambayo inaonekana kama tekinolojia inachukua nafasi ya mungu kwa kiasi fulani  inaendelea kujitokeza ..wanandoa fulani nchini marekani baada ya kukaa kwa zaidi ya miaka mitatu bila kupata mtoto na baada ya vipimo ikagunduliwa kwamba haitakuwa rahisi kwao kupata mtoto ni hiki  hapa walichokifanya,,

Baada ya kuona hivyo wakafanya utaratibu wa kupandikiza mimba ambayo tayari ilikuwa imeshaanza kukua  katika tumbo la uzazi wa binti yake na akapandikiziwa mama mzazi wa binti huyo kwa mkataba maalumu na mtoto huyo ambaye anatarajiwa kuwa binti atazaliwa mwezi ujayo yaani mwezi wa pili 2014

je watanzani utaratibu huu ukipitishwa hapa kwetu upendo utaongezeka au utazidi kupoa.....lakini pia je mbele ya mungu hii ni saw?


No comments:

Post a Comment