Monday, April 28, 2014

KWA NINI NDOA ZA LEO NI FULL MAJANGA???

Hakuna maendeleo yoyote kwa kujivunia ambayo unaweza kuyapata kama huna mahusiano mazuri na ndugu jamaa na marafiki ,lakini leo tuangalie kidogo tuu upande wa mahusiano ambayo yanaendeleza kizazi duniani kwa maana ya kwamba mume na mke ambao kwa hiyar yao wenyewe wanaamua kufunga ndoa na kuwa kitu kimoja, wakiwa na mawazo mengi ambayo huwenda walikuwa wanayawaza wakati wa ukapera.

   Lakini  je hizi hapa chini diyo sababu ya ndoa nyingi za vijana wa leo kuvunjika?
1-Umri wao unakuwa bado mdogo?
2-Maadili yao hayako sawa?
3-Matarajio yao  yanakuwa nje ya uwezo wao?
4-Utandawazi unarubuni bongo zao?
5-Wanatamani uhuru zaidi?
6-Wanakwepa majukumu yao kama wana ndoa?
7-Hawakuwa tayari kuingia kwenye ndoa?
8-Tamaa za kimwili ziliwalaghai?
9-Matatizo ya kiuchumi?
10-Ndoa zao zinajengwa na akili zao na si mungu?
Toeni maoni yenu wakuu ili tuone nanma ya kutoka hapa tulipo kama jamii....kwa sms 0756 787 089
WADADA WA LEO

No comments:

Post a Comment