Friday, September 12, 2014

MAHUSIANO YA LEO NI KAMA NDOTO YA MCHANA

Habari wanajamvi!!!!!!
         Napenda kutumia fulsa hii kukusalimu lakini pia kuzungumza japo kwa uchache wake juu ya mahusiano yako na yangu katika dunia ya leo ya kisasa japo mimi siamini sana huu usasa.
        Leo ni siku nzuri ambayo huenda umepata mchumba mpya,mpenzi mpya,ama unayofuraha kwa sababu umekutana na mwenzako mkaamua kuwa kama mlivyozaliwa na hatimaye mkaamua muburudisha akili zenu na miili yenu,ni jambo jema kama lilifanyika kwa watu sahihi,muda sahihi na kwa usahihi wake,kama ilikuwa hivyo hongera kwa kutimiza takwa takatifu la mungu na kama ni kinyume chake poleni,
         Kwa nini tunasema  mahusiano ya leo ni kama ndoto ya mchana ni jibu ni jepesi kwa sababu mahusiano ya leo hayaaminiki hata kidogo,hata kwa wale waliojaribu kujiamini wao, wamejikuta wenzi wao hawaaminiki,kwa hiyo hii inajenga uhalali wa kwamba mahusiano ya kileo ni kama ndoto ya mchana.,lakini pia inajengwa na dhana hii, leo ukikutana na binti au kijana akatamka kwamba anakupenda,hilo neno nakupenda limebeba maana nyingine kabisa tena maana ovu,huenda anakutamani ama anataka kukuumiza tu moyo wako au anataka aondoke na roho yako,yote matatu yanawezekana na mifano yake ipo wazi kabisa na wewe unayesoma hapa ushahidi huo unao,wangapi umewadanganya,wangapi uliwambia unawapenda kumbe unawatamani,,,,,,,,,,jibu unalo na pigia mstari....
          Lakini mimi ningependa niwasihi kitu kimoja wakubwa kwa wadogo,mapenzi yapo,ngono zembe zipo na magonjwa yapo,lakini bado binadamu sisi tunaendeleza hayo yote matatu kwa kasi mpya na ari mpya.mapenzi siyo kitu kibaya mapenzi ni afya ya mtu,mapenzi yanaleta uhusiano chanya tena wenye tija ya kuongeza uzao wa dunia kama yakitumika kwa ufasaha wake.lakini mtu wa kulinda utu wako na afya yako ni jukumu lako la kwanza wewe binafsi,usiruhusu mtu mwingine aamue hatima ya afya yako wala utu wako,ulizaliwa mtu huru na unao uhuru wa kulinda afya yako na ikiwezekana ikipokwa na mtu yeyote idai kwa nguvu na mungu atakulinda.
     Leo umdhaniaye ndiye kumbe siye,basi leo katika mahusiano usitumie hisia,dhana,nenda na fact ili uwe na mwisho bora,,,wanawake waaminifu wapo na wanaume waaminifu wapo japo kwa uchache wao lakini mwombe mungu akusaidie katika hilo,,,,
             Barikiwa sana na asante kwa kusoma

LAZIMA UTIMIZE WAJIBU WAKO CHANYA KABLA YA KUTENGANA NA DUNIA HII

Habari wadau,
          Napenda kuwasalimu katika jina la muumba mwenyezi aliyetujalia siku hii ya leo,jina lake lihimidiwe.napenda pia kutumia nafasi hii adimu kushirikisha mawazo yangu kwenu wadau juu ya utaratibu wa binadamu kufanya yale yampasayo kwa hiyari yake bila shuruti.
      Kama tunavyofahamu kwamba kila binadamu alipewa siku za kuishi hapa duniani na mungu mwenyezi,hilo halina ubishi wale mjadala wake si mpana sana kwa binadamu yoyoye anayepumua pumzi hii anajua hilo kwa uzuri zaidi,lakini pamoja na kujua hilo binadamu wa leo amesahau wajibu wake,kwake mwenyewe,kwa binadamu wenzake kwa viumbe wengine na zaidi amesahau mpaka wajibu wake kwa mungu wake,
      Matokeo ya ukengeufu huo wa binadamu umeletelezea matatizo makubwa yasiyomithilika kwa binadamu na viumbe wengine,lakini chanzo kikubwa ni binadamu huyu huyu ambaye alibarikiwa UTASHI na mwenyezi mungu,mungu alimpa kila binadamu kipawa chake na shabaha ya kukupa kipawa hicho ilikuwa ni ili uweze kukitumia vema kwa manufaa ya mungu wako na viumbe wengine pia maana mungu aliweka mahitajiano ili kila awaye aheshimiwe kwa kipawa chake na mwingine.
      Leo tunalotatizo katika taifa letu la tanzania,watu wanafanya kazi zisizo zao yaani kwa lugha ya mtaani wamevamia fani za watu,si kwa sababu hawajui ila ni kwa sababu ya tamaa za miili yao na washirika wao,lakini niwakumbushe kitu siku ya hukumu ya haki utaulizwa kwanini hukufanya kazi niliyokutuma,na jibu lake unalo na utahukumiwa kwa hilo.kwa kile ambacho mungu alikutunuku basi kitumie vema maana kabla ya kuondoka kwako hapa duniani huko uendako hakuna nafasi tena ya kutenda yale uliyoshindwa kuyatenda duniani kwa haki,ukimaliza basi yatosha,subiri hukumu yako ya haki kwa matendo yako,
       Ndugu zangu,kila mtu anatenda jambo,lakini si kila jambo ni jambo jema machoni pa mungu,jitahidi sana utende mambo yako kwa ukubwa wa hekima uliyojaliwa kuwa nayo na pia upime ukuu wa matendo yako kwa jamii yako,maana huwezi kutenda jema machoni pa mungu ingali umemtenda vibaya jirani yako,.
         Kiongozi wa bunge la katiba Mh. sitta  lazima atende mambo yake kwa hekima,tanzania na watanzania machozi yao yatakuwa juu yake,maana ndani ya moyo wake anashuhudiwa uovu unaoendelea, lakini kutokana na kiburi cha uzima au uchanga wa kumjua mungu anashupaa shingo.lazima tufanya jambo la kheri kabla ya kuondoka kwetu duniani.
                  Asante kwa kusoma