Friday, September 12, 2014

LAZIMA UTIMIZE WAJIBU WAKO CHANYA KABLA YA KUTENGANA NA DUNIA HII

Habari wadau,
          Napenda kuwasalimu katika jina la muumba mwenyezi aliyetujalia siku hii ya leo,jina lake lihimidiwe.napenda pia kutumia nafasi hii adimu kushirikisha mawazo yangu kwenu wadau juu ya utaratibu wa binadamu kufanya yale yampasayo kwa hiyari yake bila shuruti.
      Kama tunavyofahamu kwamba kila binadamu alipewa siku za kuishi hapa duniani na mungu mwenyezi,hilo halina ubishi wale mjadala wake si mpana sana kwa binadamu yoyoye anayepumua pumzi hii anajua hilo kwa uzuri zaidi,lakini pamoja na kujua hilo binadamu wa leo amesahau wajibu wake,kwake mwenyewe,kwa binadamu wenzake kwa viumbe wengine na zaidi amesahau mpaka wajibu wake kwa mungu wake,
      Matokeo ya ukengeufu huo wa binadamu umeletelezea matatizo makubwa yasiyomithilika kwa binadamu na viumbe wengine,lakini chanzo kikubwa ni binadamu huyu huyu ambaye alibarikiwa UTASHI na mwenyezi mungu,mungu alimpa kila binadamu kipawa chake na shabaha ya kukupa kipawa hicho ilikuwa ni ili uweze kukitumia vema kwa manufaa ya mungu wako na viumbe wengine pia maana mungu aliweka mahitajiano ili kila awaye aheshimiwe kwa kipawa chake na mwingine.
      Leo tunalotatizo katika taifa letu la tanzania,watu wanafanya kazi zisizo zao yaani kwa lugha ya mtaani wamevamia fani za watu,si kwa sababu hawajui ila ni kwa sababu ya tamaa za miili yao na washirika wao,lakini niwakumbushe kitu siku ya hukumu ya haki utaulizwa kwanini hukufanya kazi niliyokutuma,na jibu lake unalo na utahukumiwa kwa hilo.kwa kile ambacho mungu alikutunuku basi kitumie vema maana kabla ya kuondoka kwako hapa duniani huko uendako hakuna nafasi tena ya kutenda yale uliyoshindwa kuyatenda duniani kwa haki,ukimaliza basi yatosha,subiri hukumu yako ya haki kwa matendo yako,
       Ndugu zangu,kila mtu anatenda jambo,lakini si kila jambo ni jambo jema machoni pa mungu,jitahidi sana utende mambo yako kwa ukubwa wa hekima uliyojaliwa kuwa nayo na pia upime ukuu wa matendo yako kwa jamii yako,maana huwezi kutenda jema machoni pa mungu ingali umemtenda vibaya jirani yako,.
         Kiongozi wa bunge la katiba Mh. sitta  lazima atende mambo yake kwa hekima,tanzania na watanzania machozi yao yatakuwa juu yake,maana ndani ya moyo wake anashuhudiwa uovu unaoendelea, lakini kutokana na kiburi cha uzima au uchanga wa kumjua mungu anashupaa shingo.lazima tufanya jambo la kheri kabla ya kuondoka kwetu duniani.
                  Asante kwa kusoma 

No comments:

Post a Comment