Haijalishi ni kiasi gani cha maneno unasema bali ni mhimu kujua katika maneno yako yote ni maneno yapi chanya...karibu katika siasa za tanzania na afrika,
Kama yalivyo mabara mengine basi na afrika nayo ina mambo yake ambayo hayapishani sana na mfumo wa dunia na yale yanayofanywa na dunia nyingine kwa maana ya mabara ya amerika zote,ulaya,asia na australia,lakini katika afrika siasa zake ni za aina zake yaani watu kuuana,wizi wa kura,kubambikizia kesi wagombea,mfumo dume,na zaidi hakuna haki na uwazi katika kupiga kura mpaka kutangazwa matokeo..hii ni hali halisi.na machafuko mengi chanzo ni hapo,
ACT-chama kipya,karibuni katika uwanja ule ule wa siasa ila mkiwa na jezi mpya.matumaini ya watu ni kuona maneno yenu yanaakisi vitendo vyenu,mumewaaminisha watu hivyo na watu wanalo tumaini hilo,haijalishi ni kubwa kiasi gani au dogo kiasi gani,,maana bado mtafanya siasa za muda wenu na sababu ikiisha mtakaa pembeni mpishe kizazi kingine.
Fanyeni lililo jema ili mkumbukwe kwa uzuri huo muda wenu "ukikwisha" friend of mine from kenya told me that.
![]() |
ZITO,S TEAM |
Huna sababu ya kuwa wa kwanza au wa mwisho maana taifa linajengwa kila siku,shabaha ni kufanya mambo sahihi kwa masilahi ya taifa letu,,kinyume chake ni hukumu zote mbili duniani na mbinguni