Saturday, March 14, 2015

TUNAHITAJI NEEMA YA MUNGU KUPONA

Habari ndugu wanajopo,,,
        Tanzania nchi yangu,tanzania nyumbani kwangu kwa daima katika maisha yote ya huu mwili wangu,nakupenda sana,,
        Leo naona kuna jambo moja tu ambalo inabidi mungu wetu tunayemwamini aingilie kati ili nchi yetu indelee kuwa na amani na mshikamano wa kutosha na kuigwa na jamii nyingine zinazotuzunguka.
      Tanzania kwa sasa tuna mambo makubwa mawili mbele yetu ambayo yataamua amani wa taifa letu..KATIBA MPYA INAYOPENDEKEZWA NA UCHAGUZI MKUU,kupigia kura ya maoni katiba inayopendekezwa ni april 30 na uchaguzi mkuu ni october 2015,lakini mpaka sasa majimbo yaliyoandikishwa wapiga kura si zaidi ya matatu,,,hii ni hatari,tena siyo hatari ndogo kwa amani ya taifa letu,
     Ndugu rais katangaza yeye badala ya tume ya uchaguzi,ukiacha kuwageuga umoja wa vyama vya siasa yale waliyokubaliana kunduchi dar es laam na baadaye dodoma,na haki kuwageuka kwa sababu yeye ndiyo mkuu wa nchi labda aliona kuna jambo la mhimu zaidi kuliko makubalianao hayo sisi hatuwezi kujua,,,ila ninachokifahamu mimi ni lazima watanzania tumwombee rais wetu ili genge la mafisadi lisifanye mashinikizo kama haya ambayo yanaliweka taifa letu njia panda.
    Uchaguzi mkuu ni chanzo cha vurugu kubwa duniani kama kutakuwa hakuna maandalizi ya uhakika na yanayoaminika na jamii iliyokubwa,nchi nyingi za afrika zimekumbwa na machafuko kutokana na jambo hili......
 tafakari,,, chukua hatua,,,,

JESUS SAVE

No comments:

Post a Comment