Salamu ndugu,
Napenda kutumia nafasi hii kuwasalimu ndugu zangu katika mungu mwenyezi mwenye enzi na mwanawe pekee mfufuka kristo yesu salam,leo ni siku bora tuliyopewa naye basi ya tupasa kumshukuru kwa uwezo wetu wote.
Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza,afya bora ya akili ni kuishi maisha yenye kusudi chanya.huenda ukawa na ukakasi wa kufahamu afya ya akili ni nini,Mungu wakati anaamua kuumba binadamu kwa mfano wake alikuwa na kusudi chanya juu ya binadamu huyu na ndio maana alikuambia nenda duniani ukatawale..kinachotawala siyo mwili bali akili,na hii akili ni kitu kisichoonekana bali tunaona matokeo yake, kama ilivyo kwa Mungu, pia Mungu haonekani lakini hakuna ubishi kwamba kazi zake au matokeo ya uwepo wake yapo wazi kwa kila kiumbe.
Basi afya ya akili inatokana na binadamu huyu kujaza akili yake mawazo chanya au mawazo hai na siyo mawazo mufu,binadamu anayeamua kuwaza hasi, tafsiri yake maisha yake yatakuwa na kusudi hasi,kwa mfano mtu anayewaza kujenga nyumba ya tembe,,linaanza wazo anaijenga ile nyumba katika ulimwengu mkuu au alimwengu wa wazo kuu na kisha baadaye anakuja kuhamishia katika ulimwengu wa kifizikia yaani katika dunia hii tuishiyo.kwa hiyo uwezo wa huyu mtu wa mawazo aliyoamua kuondoka nayo ni haya ya kujenga nyumba ya tembe,japo alipewa chaguo la mawazo mengi ila yeye aliamua kuondoka na hilo maana mengine aliona magumu.
Lakini zaidi,binadamu huyu huyu wa jiografia nyingine aliondoka na wazo la ghorofa mia tatu kwenda juu.yeye aliondoka na hilo akaona ndiyo linamfaa na hatimaye amelitekeleza wazo lake katika dunia hii hii tuishio..kwa hiyo afya ya akili inatekelezwa na mashineli inayoitwa mwili pamoja na milango yake yote ya fahamu inapelekea wazo kuwa kitu halisi.
Ili uishi vizuri katika ulimwengu wako wa kifizikia lazima uishi kwa kusudi chanya katika ulimwengu wako wa wazo kuu(kiroho)ufanikiwe huko kwanza ndipo uje ufanikiwe pia katika ulimwengu wako wa kuonekana.
Kumbuka, kuwa na wazo dogo siyo kosa ila ni matokeo ya kile ulichokichukua katika ulimwengu wa kiroho,kwa lugha nyingine bado mafanikiao yako katika ulimwengu wa kiroho ni ya kujikongoja na hiyo inadhihirisha kwamba,unavyoitwa na kocha mkuu wa team hii ya wazo kuu(MUNGU) na unapangwa kwenye first eleven yake,huchezi kwa umakini na hatimaye hufungi goli mpaka dakika 90, matokeo yake ni kutoka nje ukiwa hoi na point tatu umekosa,..
NIMALIZE LEO KWA KUSEMA,HAKUNA SABABU YOYOTE ITAYOKUZUIA KUWA NA AFYA BORA YA AKILI YAKO,ILA UPO UCHAGUZI WA HIYARI AMA UCHAGUE KUCHEZA KWA BIDII AU UCHAGUE KUCHEZA KWA MAZOEA...(mazoea ni rafiki na mwili wako bali bidii ni rafiki na akili yako)
Saturday, June 27, 2015
Friday, June 19, 2015
POLE YAKO MWANANCHI UNAYENUNULIWA KWA FEDHA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI
Salama ndugu,
Kwanza kabisa napenda kumshukuru mungu kwa wakati huu tena uliokubalika,wengi walitamani kuiona leo lakini hawajaiona si kwa sababu wewe na mimi tu wema sana bali ni kwa neema yake tu ya ajabu juu yetu sisi viumbe tusio na shukurani kwa Mungu wetu.
Katika ulimwengu wa kipepari kama huu tulio nao sasa ni rahisi sana binadamu kuuza utu wake kwa ujinga wake mwenyewe,ujinga ni hatua, maana ukiambiwa mjinga leo, kesho na kesho kutwa mtondogoo utajifunza au utaacha kusema usichokijua. leo katika taifa letu kuna watu ambao wameacha kufikiri kwa makusudi mazima,wakikosa kazi za kufanya, wakikosa msaada wa hali na mali basi nao wanakaa chini wanasubili muujiza wa mungu.sasa mtu kama huyu kwanini asinunuliwe na mwanasiasa bepari?ambaye atamsaidia elfu mbili ya ugali wa mchana na kofia ya kuzuia jua na hatimaye atamtimizia haja zake huyu mwanasiasa ya kumpigia kura,
Kuna mifano ya wazi kabisa katika taifa letu,mtu anajiita msomi eti naye analalamika ajira,mwizi, hana uzalendo,hajiamini,na zaidi anageuka kuwa bingwa wa kutumika na wanasiasa uchwara eti kwa sababu tu hana fedha,hawa ndiyo wanao dhalilisha hii kada ya wasomi waonekane sifuri,japo siyo wote ila katika uwingi wao,ukiona kuna msomi anaamini kwamba ccm italeta mabadiliko,huyu mtu mchunguze mara mbili ama anamaslahi ya moja kwa moja au ni bepari wa kutupwa anataka kulinda na kutetea masilahi yake au alienda shule ila hakuelimika ipasavyo.huwezi kumkosa katika makundi haya matatu.
Nchi hii imekuwa na umasikini wa aibu kwa sababu tu utawala uliopo hauna nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa watanzania,haiwezekani tanzania kukosa maji safi na salama miaka 50 ni chini ya asilimia 25% ya watanzania wote,uhakika wa chakula ni wa mashaka ,mungu asipoleta mvua tnasaidiwa mpaka na vietinam mchele,i hali bonde moja tu la IHEFU au MBALALI mbeya linaweza kulisha taifa zima,unakuta mtu anakuwa shabiki wa jambo asilolijua kwa ujinga wake anajiona anajua sana,na hii ndiyo mbinu inayotumiwa na ccm kuwahada wananchi,tunakosa elimu bora ili uelewa wetu uwe finyu na wao na familia zao wazidi kututawala.
Ukipenda,, muda ni sasa,jiulize maisha yako yanaongozwa na nani?mwisho wako nani anao mikononi mwake?historia yako itajengwa katika misingi ipi?na je maendeleo ni kuwa na fedha tu?msingi wa maendeleo ni upi katika nchi zilizoendelea?ukipata majibu sahihi au majibu yasiyo sahihi bado endelea na safari yako ya ujinga.wapo watakao fanya baadala yako katika kila jambo.
Hakuna kiasi cha fedha kinacholingana na thamani yako,usikubali kununuliwa kwa pilau na fulana,nenda kapige kura yako maana ni haki yako ya msingi,mchague kiongozi unayeamini anao uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika eneo lako,ukweli ni huu,,shida zote na matatizo yote katika nchi hii mwasisi wake ni ccm,ila kama unaridhika na hayo yote nenda kawapigie tena kura ni haki yako ya kikatiba...katiba inawalinda na kuwapa haki wote hata (wale wenye akili za kuvukia barabara)
MUNGU IBARIKI TANZANIA,TUJALIE AMANI NA UWAPE HEKIMA WATAWALA HAWA NA SAA YA MABADILIKO II KARIBU

Subscribe to:
Posts (Atom)