Salamu ndugu,
Napenda kutumia nafasi hii kuwasalimu ndugu zangu katika mungu mwenyezi mwenye enzi na mwanawe pekee mfufuka kristo yesu salam,leo ni siku bora tuliyopewa naye basi ya tupasa kumshukuru kwa uwezo wetu wote.
Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza,afya bora ya akili ni kuishi maisha yenye kusudi chanya.huenda ukawa na ukakasi wa kufahamu afya ya akili ni nini,Mungu wakati anaamua kuumba binadamu kwa mfano wake alikuwa na kusudi chanya juu ya binadamu huyu na ndio maana alikuambia nenda duniani ukatawale..kinachotawala siyo mwili bali akili,na hii akili ni kitu kisichoonekana bali tunaona matokeo yake, kama ilivyo kwa Mungu, pia Mungu haonekani lakini hakuna ubishi kwamba kazi zake au matokeo ya uwepo wake yapo wazi kwa kila kiumbe.
Basi afya ya akili inatokana na binadamu huyu kujaza akili yake mawazo chanya au mawazo hai na siyo mawazo mufu,binadamu anayeamua kuwaza hasi, tafsiri yake maisha yake yatakuwa na kusudi hasi,kwa mfano mtu anayewaza kujenga nyumba ya tembe,,linaanza wazo anaijenga ile nyumba katika ulimwengu mkuu au alimwengu wa wazo kuu na kisha baadaye anakuja kuhamishia katika ulimwengu wa kifizikia yaani katika dunia hii tuishiyo.kwa hiyo uwezo wa huyu mtu wa mawazo aliyoamua kuondoka nayo ni haya ya kujenga nyumba ya tembe,japo alipewa chaguo la mawazo mengi ila yeye aliamua kuondoka na hilo maana mengine aliona magumu.
Lakini zaidi,binadamu huyu huyu wa jiografia nyingine aliondoka na wazo la ghorofa mia tatu kwenda juu.yeye aliondoka na hilo akaona ndiyo linamfaa na hatimaye amelitekeleza wazo lake katika dunia hii hii tuishio..kwa hiyo afya ya akili inatekelezwa na mashineli inayoitwa mwili pamoja na milango yake yote ya fahamu inapelekea wazo kuwa kitu halisi.
Ili uishi vizuri katika ulimwengu wako wa kifizikia lazima uishi kwa kusudi chanya katika ulimwengu wako wa wazo kuu(kiroho)ufanikiwe huko kwanza ndipo uje ufanikiwe pia katika ulimwengu wako wa kuonekana.
Kumbuka, kuwa na wazo dogo siyo kosa ila ni matokeo ya kile ulichokichukua katika ulimwengu wa kiroho,kwa lugha nyingine bado mafanikiao yako katika ulimwengu wa kiroho ni ya kujikongoja na hiyo inadhihirisha kwamba,unavyoitwa na kocha mkuu wa team hii ya wazo kuu(MUNGU) na unapangwa kwenye first eleven yake,huchezi kwa umakini na hatimaye hufungi goli mpaka dakika 90, matokeo yake ni kutoka nje ukiwa hoi na point tatu umekosa,..
NIMALIZE LEO KWA KUSEMA,HAKUNA SABABU YOYOTE ITAYOKUZUIA KUWA NA AFYA BORA YA AKILI YAKO,ILA UPO UCHAGUZI WA HIYARI AMA UCHAGUE KUCHEZA KWA BIDII AU UCHAGUE KUCHEZA KWA MAZOEA...(mazoea ni rafiki na mwili wako bali bidii ni rafiki na akili yako)
No comments:
Post a Comment