Friday, June 19, 2015

POLE YAKO MWANANCHI UNAYENUNULIWA KWA FEDHA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI

Salama ndugu,
        Kwanza kabisa napenda kumshukuru mungu kwa wakati huu tena uliokubalika,wengi walitamani kuiona leo lakini hawajaiona si kwa sababu wewe na mimi tu wema sana bali ni kwa neema yake tu ya ajabu juu yetu sisi viumbe tusio na shukurani kwa Mungu wetu.
      Katika ulimwengu wa kipepari kama huu tulio nao sasa ni rahisi sana  binadamu kuuza utu wake kwa ujinga wake mwenyewe,ujinga ni hatua, maana ukiambiwa mjinga leo, kesho na kesho kutwa mtondogoo utajifunza au utaacha kusema usichokijua. leo katika taifa letu kuna watu ambao wameacha kufikiri kwa makusudi mazima,wakikosa kazi za kufanya, wakikosa msaada wa hali na mali basi nao wanakaa chini wanasubili muujiza wa mungu.sasa mtu kama huyu kwanini asinunuliwe na mwanasiasa bepari?ambaye atamsaidia elfu mbili ya ugali wa mchana na kofia ya kuzuia jua na hatimaye atamtimizia haja zake huyu mwanasiasa ya kumpigia kura,
  Kuna mifano ya wazi kabisa katika taifa letu,mtu anajiita msomi eti naye analalamika ajira,mwizi, hana uzalendo,hajiamini,na zaidi anageuka kuwa bingwa wa kutumika na wanasiasa uchwara eti kwa sababu tu hana fedha,hawa ndiyo wanao dhalilisha hii kada ya wasomi waonekane sifuri,japo siyo wote ila katika uwingi wao,ukiona kuna msomi anaamini kwamba ccm italeta mabadiliko,huyu mtu mchunguze mara mbili ama anamaslahi ya moja kwa moja au ni bepari wa kutupwa anataka kulinda na kutetea masilahi yake au alienda shule ila hakuelimika ipasavyo.huwezi kumkosa katika makundi haya matatu.
     Nchi hii imekuwa na umasikini wa aibu kwa sababu tu utawala uliopo hauna nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa watanzania,haiwezekani tanzania kukosa maji safi na salama miaka 50 ni chini ya asilimia 25% ya watanzania wote,uhakika wa chakula ni wa mashaka ,mungu asipoleta mvua tnasaidiwa mpaka na vietinam mchele,i hali bonde moja tu la IHEFU au MBALALI mbeya linaweza kulisha taifa zima,unakuta mtu anakuwa shabiki wa jambo asilolijua kwa ujinga wake anajiona anajua sana,na hii ndiyo mbinu inayotumiwa na ccm kuwahada wananchi,tunakosa elimu bora  ili uelewa wetu uwe finyu na wao na familia zao wazidi kututawala.
    Ukipenda,, muda ni sasa,jiulize maisha yako yanaongozwa na nani?mwisho wako nani anao mikononi mwake?historia yako itajengwa katika misingi ipi?na je maendeleo ni kuwa na fedha tu?msingi wa maendeleo ni upi katika nchi zilizoendelea?ukipata majibu sahihi au majibu yasiyo sahihi bado endelea na safari yako ya ujinga.wapo watakao fanya baadala yako katika kila jambo.
   Hakuna kiasi cha fedha kinacholingana na thamani yako,usikubali kununuliwa kwa pilau na fulana,nenda kapige kura yako maana ni haki yako ya msingi,mchague kiongozi unayeamini anao uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika eneo lako,ukweli ni huu,,shida zote na matatizo yote katika nchi hii mwasisi wake ni ccm,ila kama unaridhika na hayo yote nenda kawapigie tena kura ni haki yako ya kikatiba...katiba inawalinda  na kuwapa haki wote hata (wale wenye akili za kuvukia barabara)
MUNGU IBARIKI TANZANIA,TUJALIE AMANI NA UWAPE HEKIMA WATAWALA HAWA NA SAA YA MABADILIKO II KARIBU

No comments:

Post a Comment