Tuesday, January 5, 2016

MAHAKAMA YAZUIA KWA MUDA BOMOA BOMOA KINONDONI

Mahakamu kuu kitengo cha ardhi,imetoa agizo kwa serikali kusitisha bomoabomoa iliyokuwa inaendelea mpaka mchana wa tarehe wa leo 5/01/2015 katika mitaa ya magomeni na kinondoni,mpake kesi ya msingi ifikie uamuzi.
     Kwa mtazamo wangu mahakama imefanya kazi yake vizuri,lakini kesi yenyewe ya msingi  na madai yake kiukweli si ya msingi kisheria,madai ya raia hawa wahanga na mbunge wao wa kinondoni kwa tiketi ya cuf, yanapunguza makali ya tukio lenyewe lakini si msingi wa kuzuia zoezi,

  Hoja yao ya kwanza wananchi wapewe muda wa kujiandaa,hoja ya pili watu wapewe maeneo mbadala ya kuishi ili wapishe zoezi kuendelea.
     Kwa hoja hizi maana yake wakazi wenyewe wanajua maeneo wanapoishi si maeneo halali na si salama kwa maisha yao pia, kwa hulka ya serikali hii ya hapa kazi tu I hope zoezi lao litaendelea maana hata rais wetu si rafiki sana na justice.
   Lakini pia hili zuio halina urafiki na maeneo mengine yaliyowekwa x na yanayoendelea kuwekwa x katika jiji la dar es salaam na kwingineko.


             LET’S KEEP ON WAITING GUY'S ONFIRE.

No comments:

Post a Comment