Tuesday, April 12, 2016

NINI MAANA YA WAKATI WA MAAMUZI MAGUMU

salama ndugu zangu!!!!
  Tumaini langu ni kubwa kwa mungu wetu aliyetupa tena nafasi ya kuiona leo,nasema asante hata kwa niaba ya msomaji wangu huyu,ambaye labda alisahau kukuambia asante nyakati za asubuhi.endelea......
      
       "Moja kati ya sifa mhimu ya kiongozi ni kufanya maamuzi magumu,i hali anazo taarifa nyingi mkononi zenye maoni yanayokinzana"moja ya kipimo ukitaka kujua kiongozi bora..

Leo nimeona tuzungumze jambo moja mhimu sana katika maisha yetu ya kila siku,na jambo lenyewe ni maamuzi,watu wengi tumekuwa tukichelewa kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yetu kutokana  tu na hofu ya mabadiliko,lakini ukishafanya maamuzi, majuto yanageuka na kujilaumu kwanini ulichelewa kufanya maamuzi mapema maana ulipo baada ya maamuzi yako ni bora zaidi.

  Kila aina ya maamuzi yana ghalama zake ambazo lazima zibebwe ama na mfanya maamuzi,au mtu wa pili na  wa tatu.lakini kitu kinachobeba msingi wa maamuzi ni kusudi la kufikia matokeo chanya yenye tija kwa jamii kubwa zaidi,hii imepelekea wengine kushindwa kuendana au kuzikabili gharama hizo za maamuzi ambazo zimegawanyika katika makundi kadhaa,moja mali au fedha,hisia(msongo wa mawazo) upweke,aibu,n.k...lakini hakuna maendeleo yaliyokuja bila kufanya maamuzi yanayokinzana na walio wengi ambao kikawaida hufikiri kawaida,kwa jinsi hiyo popote ulipo wewe ni kiongozi wa akili yako na jamii ingine ama familia na kuendelea, basi ni wasaa wako wa kufanya maamuzi sahihi yatakayo chora dira ya kizazi chako.

 Lakini pia kiongozi bora hufanya tathimini ya maamuzi yake na kupokea matokeo yake na kuyabeba mwenyewe bila kusaidiwa na awaye,kama alifanya makosa basi lazima awe tayari kulikabili hilo na kuona namna bora zaidi ya kusonga mbele.
  viongozi wengi wa afrika  wameleta homa ya afrika,hawafanyi maamuzi yenye tija kwa mataifa yao na hii imepelekea raia wake kuzoea njia za mkato, na wakati wachache wakifanya maamuzi sahihi huonekana wamekosea na hukemewa hadharani hii haikubaliki popote duniani,lazima tubadilike kabla ya kusema fikiri nini unataka kusema na kwa nini unasema na je ni mahala sahihi lakini la zaidi je ni muda sahihi?

Usisite kufanya maamuzi magumu hata kama unazotaarifa nyingi mkononi mwako,wewe kama kiongozi kitu cha kufikiri ni maslahi mapana ya jamii yako,na
uwe tayari kupokea mawazo tofauti na maamuzi yako,na kauli thabiti huwa ni kupokea mawazo na kuyapima katika mizania inayofaa na ikiwa inafaa itatumika siku za usoni bila kubatilisha maamuzi ya awali...huyu hupimwa kama kiongozi imara na shupavu mwenye uwezo wa kusimamia maamuzi yake.ni wachache duniani....ukianza leo utakuwa miongoni mwa wale wachache.

No comments:

Post a Comment