INUA UELEWA WAKO KWA KIJIFUNZA KWA WENGINE
Salama ndugu zangu!!
Napenda kumshukuru Mungu mwenyezi aliyetupa
nafasi ya kuiona leo,pia kuwapa pole ndugu zangu wote walio katika mateso ya
dunia hii,lakini jipe moyo maana mtetezi wako yuu hai na uamzi upo juu yako
leo….endelea
Inua uelewa wako kwa kujifunza kutoka kwa
wengine,ni sentensi ndefu pia yenye maana kubwa sana na urefu wenye sawia na
urefu wake,pia inatafsiri uhalisia wa maisha ya binadamu ya kila siku.kujifunza
kumegawanyika katika makundi mawili katika mantiki yake,na wote hapa dunia tupo
katika moja ya makundi haya.
-KUJIFUNZA MAMBO
CHANYA-kila binadamu aliyepewa nafasi ya kuishi anacho cha kujifunza kutoka kwa
binadamu mwingine kwa lugha nyepesa tunaweza sema kila binadamu ni mwalimu wa
mwenzake katika upande Fulani wa ubobevu wake katika ubongo wake.wapo watu
ambao huona aibu kujinza kwa sababu wanaona aibu?yaani unayakosa maarifa
chanya kwa sababu tu Fulani atanicheka au Fulani akijua atatusumbua sana kwa
hiyo hutaki kutoa maarifa hayo kwa wengine kwa sababu tu utasumbuliwa
kufanikiwa kwa mwingine???!hizi ndizo kesi nyingi sana katika bara letu la
afrika.lakini nikutie moyo “mtu yoyote anayefikiri chanya hutenda mambo
chanya”vitu vyote unavyotumia gharama kubwa kuvipata na muda mwingine vinakamilisha
furaha yako, vilibuniwa na watu wanaofikiri chanya na wanaopenda kujifunza bila
mipaka,kwa hiyo kama akili yako unataka ifurahie kujifunza basi anza leo “kuheshimu
mawazo na vipaji vya wengine”
Hakuna uchaguzi wenye njia moja,kila uchanguzi una machaguo zaidi ya moja,
hii yote ni kipimo cha kujua ni nani hasa anajua uwezo wa akili yake na vipawa
vyake tangu kuumbwa kwake,ili uchochee kipawa chako lazima ujifunze mambo
chanya kwa upande huu wenye mawazo chanya,
Unaweza kujifunza kwa njia nyingi lakini njia bora zaidi ni ile ya
kusikia sauti yako ya ndani inakwambia nini na matokeo ya sauti hiyo igeuze
katika vitendo na watu wakuzungukao watasema wewe si wa kawaida..kuwa mpole
kiasi,yape masikio nafasi kubwa kuliko mdomo wako, kisha pongeza panapofaa
kupongeza na pia toa maoni yanayofaa kwa uwazi pale inapotakiwa ,,hatimaye
utakuwa mtu bora na jamii yako itasema huyu mtu si wakawaida na kwa matokeo ya mawazo
yako hata baada ya kuondoka mwili wako hapa duniani bado athali zako chanya
zitaishi,
KUJIFUNZA
MAMBO HASI-Mambo yote hasi ndio chanzo cha mateso na mahangaiko ya wanadamu
hapa duniani,kwa hiyo kama unatenda jambo hasi mahala ulipo basi ujue kwamba
kama siyo leo kwa mawazo yako na matendo yako ipo siku binadamu mwingine
atapata matokeo hasi kutokana na maisha yako.
Asilimia kubwa vitu vyote vyenye chembe ya uhasi ndani yake ndivyo
vinatazamwa na kuwekwa katika vyombo vya habari,magazeti,mitandandaoni na
kwingineko,lakini nini sababu?sababu kubwa binadamu wengi wanafurahia majibu ya
kawaida ya maswali yao bila kuuliza maswalimhimu ya nyongeza,na watengenezaji
wa mambo hayo hawajatoa nafasi ya maulizo kwa bidhaa zao au huduma zao
zinazodhorotesha kiwango cha kufikiri cha mwanadamu,na afrika sisi ndio wahanga
wa tatizo hili.kama hawataki kuulizwa basi kabla ya kununua huduma yake au
bidhaa yake jiridhishe kwanza mwenyewe kwa masilahi yako na kizazi chako.
Ikiwa
una uwezo wa kuuliza maswali mhimu
katika kila hatua ya maisha yako,iko siku utapata jibu sahihi na litakupelekea
kufanya jambo chanya.”hakuna dunia majibu
sahihi ya mahitaji yako mpaka utakapojua wewe unahitaji nini”kwa hiyo
kuanzia leo usiwaze hasi,maneno kama siwezi,sijui,hajui,labda Fulani,nitafanya
kesho,sina uhakika, ni maneno yanayopelekea binadamu uwaze hasi,epukana nayo
leo ili uipe nafasi akili yako
kujifunza.
Hakuna
namna bora katika kujiletea maendeleo katika dunia isiyo na huruma kama hii,
lazima ufungue kurasa mpya katika ubongo wako, uwaze na kujifunza mambo chanya
kutoka kwa binadamu wenzako na kutoka mawazo binafsi yanayoletwa na Mungu wako
kukabili mazingira yako.na hayo ndiyo mawazo bora zaidi kupata kutokea maa
na
ndiyo matokeo ya bidhaa na huduma zote hizi duniani,,,WEWE UNAWEZA ANZA LEO
No comments:
Post a Comment