Napenda kutumia fursa hii kusema hili ambalo
hasa lipo moyoni mwangu na akili yangu inaniambia hivyo,
Waafrika wengi ambao tunatoka afrika tuliopo
mahala pote pa dunia hatupendi kuambiwa
ukweli,na mr Trump anasema ukweli,amabao sisi hatuutaki.
Leo katika Tanzania yetu tunaye president
ambaye anahimiza watu wafanye kazi waache kulalamika na wafanye kazi kwa didii
zao zote na kwa uadilifu,lakini bado anaonekana hafai,mara hela hazipo,mara
nduvu ya soda mara nini,hii yote ni dalili mbaya sana kwa mwanadamu hupaswi
kulala
mika inapaswa uchukue hatua ya kutatua tatizo.
Bwana trump amejipambanua tangu kipindi
chake cha kampeni kwamba,atasema ukweli japo utawauma watu lakini ni ukweli na
ndiyo jibu sahihi la matatizo Fulani yaliyopo duniani.
Mosi..,swala la wahamiaji haramu,hajakataza
watu kuingia amerika kasikazini(marekani)bali anataka watu waingie kwa kufuata
utaratibu uliopo,na ndiyo dunia nzima inafanya,kama unataka kwenda nyumbani kwa
mtu lazima ufuate utaratibu wake ambao mara nyingi ni wa kawaida tu kama
shabaha yako ya kufika mahala hapo ni chanya.
Mbili…ugaidi na uisilam,watu hawajaelewa
hasa nini mantinki yake,middle east yote leo inapigana na imesambaratika kweli
na wanaopigana ni wenyewe kwa wenyewe,na huko kote asilimia 95% ya raia wao ni
waislam ama shia ama suni.vikundi vyote vinavyoendesha mauaji ya kutisha hapo
middle east ni muslim,amabo wanaitumia vibaya dini ya mtume,lakini mahala
wanapojificha ni kwenye mwavuli wa uislam,ndio maana trump anasema,amerika
imeshishiriki katika vita nyingi huko middle east,na wakimbizi wanapokuja ulaya
na marekani kwa wingi,bado wanahasira na marekani,kama bado wana hasira na
marekani anytime wanaweza kulipa kisasi,kama tulivyoona katika milipuko mingi
ya kujitoa mhanga marekani na ulaya wanaohusika ni watu wenye asili ya middle
east,na wanaoamini katika uislam japo si waislam halisi,anasema amani itafutwe
kwao,misaada iende kwao ili waelewane kwanza wenyewe na wale wanaotaka kwenda
marekani waende kwa sababu za msingi,ukitazama kwa jicho la kawaida huwezi
kuona mantiki ya hili.
Tatu…Afrika kwanini watu wake ni masikini na
wanakimbilia marekani na kufanya uwekezaji kule badala ya kuja kwao wawekeze?kwa
mtazamo wangu hata kesho wangerudishwa wote,waje tulijenge bara letu,maana
hayupo mtu atajenga bara letu kama wenyewe
tunakimbia,na ni jambo jepesi tu kuelewa kwamba katika zama hizi za
maendeleo makubwa ya dunia,kuwa na nchi ambayo inategemea misaada kwa zaidi ya
asilimia 50% ni aibu,tena aibu sana.tumuunge mkono rais yoyote anayehimiza watu
wafanye kazi,wawe waadilifu,wawe na uzalendo na mataifa yao.
Mwisho msiye mtaka kaja,presidenti pombe
bahati nzuri ameanza kutuzoesha kuisha maisha halisi siyo ubabaishaji kama
awali,fanya kazi ndiyo ule tena kazi halali,na Bwana mkubwa trump kuanzia
January 2017 misaada mingi sana itakoma na atafanya yale anayoona yana masilahi
kwa marekani..so tufunge mkanda wa kujiandaa kupokea mabadiliko makubwa ya
kiuchumi duniani.