Thursday, November 3, 2016

MWAKA MMOJA SI KIPIMO SAHIHI KUPIMA UKUAJI WA UCHUMI



Dr. Mpango ---WAZIRI WA FEDHA
Napenda kuwasalimu katika Mungu mwenyezi aliyetujalia uhai wake mpaka leo tuko hai na tunaandika.siku mbili tatu zilizopita rais wetu ametimiza mwaka mmoja wa kukaa madarakani pamoja na serikali yake tangu wachaguliwe na wana wanchi wa Tanzania.
  Kitu kilichojitokeza ni watu kujadili na kutoa tathimini ya ukuaji wa uchumi tangu rais aingie madarakani na kumkabidhi mikoba ya fedha yetu ya taifa Waziri Dr Mpango,.

uchumi wetu haukui kwa haraka kwa miaka mingi.na unaposema maendeleo basi unasema uchumi wa mtu mmoja mmoja na baadaye taifa,ukweli wenyewe ni mchungu lakini lazima tukubali uchumi wetu bado unasogea kwa kusua sua sana.
ENG..James Mbatia......WAZIRI KIVURI WA FEDHA
  Na sababu zipo nyingi mno ,lakini nitazitaja chache ili tuende sawa hata wale amabao hupenda ushabiki basi wafanye ushabiki wakijua kwamba hali halisi ikoje katika maisha ya watu mtaani na mikoba ya serikali haiko sawa kifedha kwa jinsi hali ilivyo.
1-uzalishaji wetu unapungua badala ya kupanda,wa mazao na bidhaa nyingine za kawaida za majumbani.
2-bandari ni chanzo mhimu sana cha mapato yetu lakini kuna upungufu mkubwa wa mizingo,tatizo utalijua endelea..
3-utitiri wa kodi usiyosadifu hali halisi ya mtanzania na wawekezaji
4-utashi wa kisiasa usiothamini mawazo ya wachache
5-ushirikiano wetu na dunia si mzuri sana,tuna hofu tusiyoijua
6-kipaumbele chetu hakikuona hitaji la taifa kwa muda huu,serikali ya viwanda,utekelezaji wake unahitaji mipango shirikishi mingi.
  Hizo hapo juu ni sababu ambazo zilifanya tangu siku za awali tuwe na uchumi unaodorora,pia zinaendelea kufanya uchumi udorore na zitaendelea kusababisha uchumi udorore.kwa jinsi hii mwaka mmoja hauwezi kuwa kipimo cha ukuaji wetu wa uchumi,maana mipango karibu inafanana ila mbinu ndo imebadilika kidogo,sasa kama tunataka tuwe na uchumi unaokimbia lazima sababu hizo zote ziwe kinyume chake,lakini si rahisi hivyo kwa serikali hii ya ccm kuyafanya hayo.
  Serikali haitaki ushauri,serikali haitaki raia wajue elimu ya uraia,serikali inafinya uhuru wa mawazo,serikali haitaki kuweka msingi wa kikatiba kutibu tatizo,badala yake wanakuja na sera,sera amabazo ni utashi wa watu kadhaa,unaona kabisa si busara kulaumu au kusifu utawala huu,maana time bado ipo huenda atasikia maoni ya watanzania.

   Ila hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda,kama hatuna sera nzuri ya kilimo,sera nzuri ya elimu,sera rafiki ya teknolojia,sera nzuri ya power(nishati),kiwanda hakijengwi tu,kiwanda kinaandaliwa mazingira chanya .

No comments:

Post a Comment