Tuesday, October 8, 2013

IKULU YAAKANUSHA KUSAINIWA KWA MSWADA WA MABADILIKO YA KATIBA NA MH.RAIS

Habari,
           Ikulu imesema kwamba muswada wa mabadiliko ya katiba uliopitishwa na bunge dodoma kwa mbwembwe kubwa na wabunge wa ccm bado haujasainiwa na mh rais,
          Imefikia hatua ya kukanusha kutokana na taarifa mbali mbali ambazo zilionekana katika vyombo vya habari mbali mbali asubuhi ya tarehe 8 october 2013.
         Inakuwa kama sinema fulani ambayo inasubiliwa kwa hamu kubwa na watazamaji wake ambao ni watanzania kwa ujumla wake...hapa kuna makundi mawili ya watanzania ambayo kila kundi wanataka kuona sinema ya aina tofauti katika kitambaa kimoja tena kwa wakati mmoja,kuna kundi la wapenda mabadiliko chanya na kundi la wapenda mabadiliko hasi,

Hawa  wote wanavutana sana lakini mshindi siku zote ukweli huwa unashinda hata ukicheleweshwa kwa nguvu ya dola bado siku utakuja kushinda.MUNGU IBARIKI TANZANIA WAJALIE HEKIMA NA BUSARA VIONGOZI WETU ILI WALIONGOZE TAIFA VEMA NA WAFANYE MAAMUZI  YA HEKIMA

No comments:

Post a Comment