Sunday, October 6, 2013

NIMEAMBIWA,,KAULI YA RAIS ILIYOJIRUDIA SANA KATIKA HOTUBA YAKE,NINI HASA MANTIKI YAKE.

Salamu ndugu zangu mabibi na mabwana,habari ya jumapili tulivu,.-----Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa rais kikwete,jopo la washauri na mama salma kwa kumshauri mheshimiwa na hatimaye kujaribu kukemea kile kinachoonekana kama ni tishio kwa amani ya taifa letu.
  Kwaninini nasema kile kinachoonekana kama ni hatari kwa taifa kumbe si hatari, bali ni uastawi wa demokrasia na utafutaji haki kwa amani kutoka kwa watawala,nimesikiliza kwa umakini sana hotuba ya rais wangu na nikaamua niirudie tena ili nisipitwe na japo neno moja.
   Katika hotuba ile kuna mambo mazuri mengi na yenye tija kwa taifa hili, Na yale ambayo watu walioamua kufikiri chanya walitaka kuyasikia basi tuliyasikia kwa asilimia kubwa japo yapo mengine muhimu hatukusikia, ila siku zote hatujachelewa tuanze pale tulipo
   Kitu mhimu leo ambacho nataka tujifunze watu wote hasa watu wa karibu na rais, watendaji na hata washauri.hili neno NIMEAMBIWA, je  neno hili lilikuja kwa bahati mbaya au lina ajenda ya siri ambayo hata wasaidizi wake hawaijui,watendaji na wasemaji wa chama dola na serikali hawaelewi mtego uliopo hapa wao wanadhani KATIBA ni kwajili ya uchaguzi wa 2015,lakini pamoja na kwamba ni mhimu kuwa na katiba bora 2015.mnasahau kwamba bila kufanya maamuzi yenye hekima na busara kwa masilahi ya taifa 2015 mtajibiwa ninyi kwenye sanduku la kura na raia hawa wa tanzania wenye umasikini wa kutupwa,
    BWANA Jakaya atakuwa anakula mafao yake na wastaafu wenzie  na kuendeleza miradi na asasi mbali mbali za kifamilia,je?Chikawe,Bulembo,Nape,Wasira,Lukuvi,Shigela,Ndugai,Mwigulu,Lusinde,pamoja na vyeti vyenu vingi,tena vyenye alama nzuri,mnachukua mambo mazito mepesi kiasi hicho?,basi kama lengo lenu ni kwenda likizo isiyo na malipo 2015 katika siasa kama Jakaya  na Bwana Pinda basi endeleeni na kutokusoma alama za nyakati ......ADUI YAKO NI YULE WA KARIBU YAKO,KILA JAMBO NA MAJIRA YAKE YATIMIAPO MAJIRA ANAYEWEZA KUBADILISHA MAJIRA HAYO NI MUNGU PEKEE.Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika



No comments:

Post a Comment