Tanzania tuadhimisha hii siku tukiwa bado na tatizo kubwa la ukeketaji kwa watoto wa kike,hii ni changamoto kubwa sana kwa viongozi wetu na jamii kwa ujumla wake,
Maana tatizo la ukeketaji ni jambo ambalo kwanza linamnyima mtu haki yake ya msingi ya kuzaliwa,pili ni jambo hatarishi maana kuna magonjwa hatarishi mengi ya kuambukiza,na pia limekuwa linawaletea madhala akina mama wakati wa uzazi.
Maoni yangu,wale wote ambao bado wanadhani ukeketaji ni mila yao wanayoiheshimu wote wamepitwa na wakati pamoja na mila zao,mabinti kataa katakata kukeketwa ukiona uazidiwa au unamheshimu mzazi basi hilo likianza kujitokeza kimbilia ofisi ya serikali ya karibu au polisi karipoti;
Si kila kitu ni kizuri kwa watu maarufu igeni vile vyenye tija kwenu na vinavyo tukuza utu wa mtoto wa kike....GOD BLESS U ALLLLLLL
No comments:
Post a Comment