Saturday, February 22, 2014

JE?UTAJIRI WA KUPINDUKIA WA WATUMISHI WA MUNGU NI MWAGAZA HALISI KWA MKRISTO WA KWELI?

Ni vema kuwa wa kweli katika ulimwengu huu ambao kila mmoja wetu amekuwa na tafsiri yake juu ya utumishi wa mungu,katika hili ni vema tukaweka  sawa kama wakristo tuliookoka, je watumishi hawa wa mungu wanapaswa kuhojiwa kwa mali zao na utajiri wao?si jambo jema kuwahoji watumishi hawa eti kwa nini wanamiliki mali nyingi,ila ni hekima kuhoji kama maisha yao yanaakisi ukristo wa kweli bila kujali mali zao,hapa ndipo ambapo yatupasa tuwaulize na kama kusema yatupasa kusema maana biblia takatifu inasema hivi;

Luka 9;23--mtu yeyote anayetaka kuwa mfuasi wangu, ni lazima ajikane nafsi yake,auchukue msalaba wake kila siku, anifuate
SIYO DHAMBI KUWA NA MALI LAKINI JE MASIKINI ANASEHEMU GANI KATIKA UPENDO WA AGAPE NA MAISHA YAKO YA KILA SIKU EWE MTUMISHI WA MUNGU?hii ni fahari ya kimungu au fahari ya kibinadamu;...

Huyu ni mchungaji mkubwa sana MAREKANI----Kama unapenda kuwa mkamilifu,nenda kauze mali yako uwape masikini hiyo fedha,nawe utakuwa na hazina mbinguni,kisha njoo unifuate(MATHAYO 19;21)

Mbweha wana mapango,na ndege wanaviota;lakini mwana wa mtu hana mahala pa  kupumzika(MATHAYO 8;20)

HILI NI MOJA KATI YA MAENEO AMBAYO YANAWAKILISHA UMASIKINI WA KUTUPWA  NCHINI INDIA,

No comments:

Post a Comment