Huenda kila mmoja wetu anamawazo chanya juu ya taifa letu la tanzania,lakini ukiona kunautofauti mkubwa ambao hauna hata dalili za maridhiano,basi lazima utilie shaka hata wazo lao la kwanza la kuwa na mawazo chanya juu ya taifa letu la tanzania,
Hakuna mahala popote dunia ambapo palikuwa na salama na palikuwa kama palivo,ila tofauti za watu katika kufikiri ndizo zilipelekea sehemu hizo kubadilika na kuwa kama palivyo,lakini mabadiliko hayo yapo ya aina mbili,mosi ni mabadiliko hanya na mbili ni mabadiliko hasi,
Nchi zote ambazo zimekuwa na msaada mkubwa kwetu zilitofautiana katika nchi zao kwa mambo mengi lakini ilikuwa ni kwa afya ya mataifa yao,walibishana kwa hoja lakini wakitanguliza masilahi ya mataifa yao,ndio maana leo tunaona maendeleo makubwa ya kiuchumi,kijamii,kisiasa na kiroho.
Sisi leo katika taifa letu,mchakato wa katiba una rafu ambazo zinaonyesha dhahili ubinafsi na uroho wa madaraka,na unaonyesha ni kwa jinsi gani watawala hawa hawana mapenzi mema na taifa hili,katiba siyo sera ya chama chochote cha siasa kwa sababu katiba inawalenga watanzania wote, walio na vyama na wale wasio na vyama.ccm ndicho chama tawala kina wabunge wengi na ndicho chenye dola,kwa mantiki hiyo hawa ndiyo ilibidi wawe mstari wa mbele kutetea masirahi ya wananchi kwa sababu waliaminiwa na watanzania,lakini hatuoni matarajio ya wananchi,tunaona mipasho na kupingana kwa hovyo kabisa baina ya tasisi na tasisi na baadhi ya viongozi wa serikali wanatofautiana katika baadhi ya mambo,na hii ni ishara kwamaba hawa jamaa si wamoja tena,
Huwezi kupingana na hoja yako mwenyewe,huwezi kuwa wa kwanza kubeza kazi ya wateule wako na kama ikitokea kweli wateule wako wamepotoka pahala basi aliyepotoa ni nyule aliyewaamini na kuwateua huyo ndiye wa kunyooshewa kidole,chama cha mapinduzi kama kuna wataalamu wa sayansi ya siasa basi inabidi wajiuzuru nafasi zao maana wameshindwa kumshauri mwenyekiti wao.lakini tukumbuke haitaishia hapo tu,tutafika mahala ambapo kutokana na mashinikizo ya viongozi wenu wakuu wa chama chenu hamtachelewa sana kujutia maamuzi ambayo mtayafanya katika andiko hili muhimu kwa taifa letu la tanzania.
Kuna maneno mawili wanapenda sana kuyatumia ,kero za muungano,,,huhitaji hata kwenda shule kujua kwamba hizi zinazoitwa kero zinatokana na udhaifu wa watawala,hawana uthubutu wa kuamua mambo kwa tija na kwa mtazamo wa baadaye,dalili za mtu ambaye hafikiri vizuri ni kufanya maamuzi nusu nusu,taifa letu la tanzania linaongoza kwa hilo.kama nchi kama marekani katiba yao inakaribia miaka mia tatu na kitu lakini bado ni imara,wao ni nani na sisi ni nani ni uzembe tu,
Kama tunataka udugu wa kweli na kuenzi muungano wetu,ama kuwe na nchi moja inayoitwa tanzania na yenye rais mmoja,ama kuwe na muungano wa nchi mbili tanganyika na zanzibar alafu tuwe na shirikisho la tanzania lenye rais mmoja,,,,hakuna hoja kwamba serikali mbili zipo,kwanza serikali mbili zimetoka wapi,ulishawahi kuona wapi ndani ya nchi moja kuna amili jeshi wakuu wawili,bendera mbili,,nyimbo za taifa mbili, hiki ni kituko tu ambacho mara nyingi kinatokea katika jamii ya watu wajinga,.
KATIBA MPYA ISIPOPATIKANA CCM WATAJIBU PAMOJA NA WINGI WAO, LAKINI HAWANA DHAMILI YA KULETA KATIBA MPYA AMBAYO ITALETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA ULAJI WAO,WATANZANIA TUACHANE NA UJINGA USIOKUWA NA TIJA,TUWAMBIE WAHESHIMU MAWAZO YETU KAMA WANANCHI....