Tuesday, June 17, 2014

DHANA YA NENO UZALENDO INAPOTOSHWA KWA ULEVI WA UMAARUFU NA MADARAKA

Habari ndugu zanguni!!

   Kuna hili jambo ambalo linaimbwa kila siku katika kituo kimoja cha radio na tv hapa kwetu tanzania,juu  y NENO  UZALENDO,nimepata shida sana kuelewa ndio maana nikaamua mawazo yangu niyalete hapa ili tujadiliane kwa kina juu ya neno hili na jinsi linavyopotoshwa ama kwa makusudi ama kwa kutokujua.

    UZALENDO ni neno lenye herufi nane tu lakini likiwa limebeba maana kubwa sana katika usitawi wa binadamu na mazingira.uzalendo ni upendo wa asili usio na sababu na unatafsiliwa katika mahusiano ya baina ya binadamu na mazingira,binadamu na binadamu ,binadamu na wanyama wengine.huo ndiyo unaitwa uzalendo na uzalendo haujengwi kwa mahubili ya matamasha au kwenye nyumba za ibada au ikulu uzalendo unajengwa kwa MATENDO CHANYA kwa viumbe wanaokuzunguka.
     Nimeona picha na sauti ya moja kwa moja kutoka kwa watu wenye umaarufu katika taifa letu kutoka pale dodoma wakati wanazindua wimbo wa uzalendo.nikajiuliza uzalendo huwa unazinduliwa?na unazinduliwa na watu maarufu!! kwa kucheza na kuimba ngonjera na nyimbo na kula pamoja ikulu,....
       Ukimwalika masikini asiye na uwezo wa kupata hata mlo wa siku moja na utakuwa umejenga uzalendo wa kweli,ukiamua kufuta chai ofisini kwenu na hela zote kununulia madawati shule zote za tanzania ambazo gharama yake ni chini ya bilion 150 utakuwa mzalendo,ukisema kuanzia leo ukikamatwa na rushwa kubwa au ndogo  unapata adhabu kali utakuwa mzalendo,ukiwataja wauza unga na wale waliokwpua hela za epa na kurudisha kimya kimya utakuwa mzalendo,ukisema wabunge wako wajadli maoni ya wananchi waliowatuma bungeni utakuwa mzalendo..
         Lakini kualikwa kuzindua uzalendo wa kinafiki si sawa,maana hata hao walioandaa tamasha hilo si wazalendo kwa matendo yao,na hao wasanii waliojinasibu hapo si wazalendo hata kidogo,baadhi yao wanajihusisha na biashara haram ya madawa ya kulevya na uchafu mwingi tu ambao hauna undungu na kitu kiitwacho uzalendo.

 Mh  rais  naamni umekuwa ukisafiri sana katika mataifa ya wenzako na kujionea mengi,ni jambo jema kusafiri na kuona mengi lengo likiwa ni kujifunza na kujifunza ni chakula cha ubongo wowote ulio hai,huko unakokwenda kweli umeona uzalendo unahubiliwa katika vyombo vya habari na huku serikali zao zikinuka rushwa na kutokutenda matakwa ya watawaliwa?naamini uwezo wako wa kusikiliza watu ni mkubwa na ni jambo jema,lakini pamoja na hayo yote naamni haukuwa muda mwafaka wa wewe kwenda kuzindua kitu ambacho macho yake yanaona karibu kiasi hiki....

   Kuna wasanii ambao hata tungo zao hazisemi kwamba wao ni wazalendo,ila wako hapo kuhakikisha masilahi yao yanapatikana na pia kuwa karibu na watawala katika bara letu la afrika kunasaidia watu kufanya maovu yao kwa maana wanao watu wa kuwalinda ..

 POLENI SANA DUNIA INAKWENDA KASI KAMA UPEPO NA AKILI ZINAKUA KILA UCHWAO---SIKU ZOTE MTU HURU NI YULE MWENYE MAWAZO HURU





         

No comments:

Post a Comment