Habari zenu ndugu,
Huenda ukawa ni mmoja kati ya watu walio karibu sana na akili yako au ukawa mbali sana na moyo wako,yote mawili yana maana kubwa sana katika maisha yako ya kila siku,msimu tunaoenda nao ni msimu wa siku kuu za krismas na mwaka mpya ,msimu ambao unahamasa nyingi sana,zifaazo kwa jamii na zile zisizofaa kwa jamii.Lazima tuhimizane kufanya yale yanayokubalika na wengi ili tutengeneze jamii yenye busara na tahaa za utu,kuna wale watakaoamua kufanya mambo mabaya kwa makusudi ya kuumiza tu wengine,labda wanataka washiriki na wengine katika maumivu yao,au wanalipiza visasi kwa siri ama wamepoteza tumaini la maisha yao kwa hiyo wanafanya lolote ili lolote litokee bila kujali matokeo yake yatakuwa hasi au chanya,watu wa jinsi hii lazima tuwaogope sana na tuwakimbie.
Huu ni wakati ambao huwezi kupima mtu kwa uharaka kiwango chake cha maisha kwa kutumia akili yako ya kawaida,maana watu wengi wamejiandaa kwa mwaka mzima,kuwa na mavazi mazuri na ya bei ghali,wamejiandaa fedha kwa ajili ya kwenda sehemu za starehe na kula vyakula vya ghalama ,kwa hiyo si jambo jepesi kuwabaini watu hawa kwa akili zetu za kawaida.
Mshirikishe Mungu ili moyo wako na akili zako zienende na kutenda kwa uweza wake mwenyewe,mshirikishe mungu kwa maombi kwa kila jambo unalotaka kufanya na Mungu wetu ni mwingi wa rehema atakuonesha njia ikupasayo na utamaliza siku kuu yako kwa amani kubwa na familia yako bila majuto ya aina yoyote ,maana kila adui yako atageuka kuwa adui wa Mungu na Mungu wetu anajibu maombi yetu,
Bwana wetu yesu kristo anasema"lihubiri neno,uwe tayari,wakati ukufaao na wakati usiokufaa,karipia,kemea,na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho"2 timotheo 4:2
Muwe na wakati mwema na pia msiishiwe na tumaini kwa bwana wetu yesu kristo maana yeye ndiye tumaini letu
No comments:
Post a Comment