Habari ndugu zangu,
Tanzanaia leo kuna jambo ambalo linaendelea na linagusa maisha ya watu wa hali ya chini kabisa na jambo hilo linalenga yale mahitaji mhimu kabisa ya binadamu, swala lenyewe linahusu makazi.
Serikali imetangaza kubomoa makazi yote ya watu nchi nzima hasa wale waliojenga sehemu zisizostahili kujengwa makazi,na tayari zoezi hili limeanza utekelezaji wake hasa katika jiji la dar es salam,ambapo katika wilaya ya kinondoni katika bonde la mkwajuni makazi zaidi ya 320 yamebomolewa,sababu zinazotolewa na serikali ukitazama kwa jicho la tatu unaona mashiko yake,lakini pia sababu hizo zinaibua maswali na hisia miongoni mwa watu juu ya utawala wa sheria na dhana ya kuheshimu utu wa mtu,
Sehemu nyingi katika taifa letu hazijapimwa,na kwa sababu tu hiyo moja inaleta maana kwamba sehemu nyingi zimevamiwa na watu,lakini je kama watu wamevamia na kuishi hapo kwa zaidi ya miaka 30,na serikali zilikuwepo na kuwa kimya,na zaidi baadhi ya watu wemepewa na hati ya makazi na serikali hizo hizo, ambapo serikali ya leo inasema hati hizo hazijulikani na ni feki.sawa tukubali hati hizo ni feki je nani anapaswa kuwajibishwa wa kwanza ni mwananchi au mtumishi wa serikali aliyetoa hati feki?utajibu wewe.
Naunga mkono kabisa kuwa, taifa linatakiwa kuwa na mipango miji inayofaa na inayoendana na ukuwaji wa dunia ,ongezeko la watu na mahitaji yake,lakini pia serikali ikumbuke kuwa serikali hizi tatu zilizopita ukiacha serikali ya mwalimu nyerere walifanya mambo ya hovyo na inabidi wawajibishwe pamoja na wananchi si haki hata kidogo mwananchi kubomolewa nyumba huku ofisa wa ardhi aliyeuza eneo husika anakuwa huru,haikubaliki.
Mwisho.....sisi wananchi pia tuache kuishi kwa mazoea,tufuate sheria na pia kila upande utimize wajibu wake kati ya serikali na raia wake.
No comments:
Post a Comment