Kwa
kuwa tuna wakati mwema mwingine ambao Mungu mwenyezi ametujalia, basi
hatunabudi kuwa waaminifu kwa huyu mungu ili tuone kusudi la kutuacha tuendelee
kuishi,maana si wote wamepata fursa hii adimu.
Naamini kabisa kuwa kila mtu awaye anawaza
kufanya jambo mwaka huu,lakini haipaswi kuwa na kiu ya kufanya jambo
tu,inapaswa hiyo kiu iambatane na uthubutu wake au utayari wa kufanya hilo
jambo.lakini pia kumbukumbu ikae sawa kidogo hapa,Yule aliyekupa kibali cha
kuuona 2016 ndiye huyo huyo ambaye anaendesha maisha yako kiroho,na wewe
umeachwa uyaendeshe kimwili tu.
Tunapoona malengo yetu hayatimii basi tujue
ya kwamba jambo hilo halijapata kibali rohoni(MUNGU)ama kwa sababu ya msingi ya
kiungu au ni mavuno ya dhambi zetu ambapo baba yake ni (SHETANI).hii yote
inakaziwa na ukweli kwamba maisha yetu hapa duniani ni ya muda mfupi sana kwa
hiyo yatupasa tutembee katika njia inayofaa ili tufanikiwe katika malengo
yetu,maana ukifanikiwa katika roho yako na utafanikiwa pia katika mambo
yatamaniwayo na macho yako.
Mwaka wa upenyo wako kama ukitembea katika
kusudi la Mungu maana tayari Mungu ameonesha kusudi jema juu yako mpaka
ukachaguliwa kuona 2016,kazi yako pekee ya kufanya ni kuishi maisha
yanayompendeza Mungu na yasiyo chukizo kwa binadamu wenzako.
Huenda akili na moyo wako vikawa vimetekwa
na matamanio ya macho yako,lakini kuanzia leo tembea katika kusudi la mungu ili
utimize malengo yako, na mwovu shetani asipate nafasi ya kukuhukumu katika
matarajio yako,kata roho ya uvivu,kukataliwa,visasi,hasira,mauti.hii yote ni
minyororo ambayo ukifumba macho ya kiroho kidogo shetani anakufunga kwayo.
Barikiwa na bwana na asante kwa kusoma
ujumbe huu,Mungu wetu akutendee na uende kupokea baraka zake,AMIN
No comments:
Post a Comment