Habari ndugu zangu,
Tumaini langu mu wazima wa siha njema,hatujakutana kwa kitambo kidogo katika jukwaa letu hili la kupashana habari na kushauriana mambo kadha wa kadha.
Tangu tuwe mbali mambo mengi yemetokea mengine ya kusikitisha na mengine ya furaha,niwape pole ya dhati wote waliohuzunishwa kwa lolote na pia niwatie moyo wale waliofurahi waendelee kuwa na bidii na mungu maana yeye ndiye muumba wa yote.
Siku zile tunakutana hapa tulikuwa chini ya rais jakaya mrisho kikwete kwa wale tulio tanzania na wale waliopo nje ya tanzania lakini wanajivunia utanzania wao popote walipo,ni kiongozi aliyetuongoza kwa miaka 10 na sasa ni rais mstaafu,ana yake mabaya na mazuri
na tutaendelea kumheshimu kama rais mstaafu.
Ameingia mr Pombe na kibwagizo chake cha ''hapa kazi tu'',ni jambo jema kuwa na kibwagizo cha jinsi hiyo ukilinganisha na nchi zetu hizi za kimasikini kuanzia mawazo mpaka ufanyaji kazi,ukisema hapa kazi tu kidogo inaamsha ari ya raia wake.lakini je kwa jinsi mifumo ya nchi hii ilivyo mr pombe atawezana nayo?
Swali hilo huenda likajibiwa na maelezo ambayo hayatakata kiu yako kwa haraka lakini yataongeza ari ya kutaka kujua zaidi.
----Urais wake unasitofahamu miongoni mwa watanzania ndani ya (ccm na kwa watanzania wote)
----Mr pombe ni mtendaji mzuri mno ila si kiongozi mzuri mno maana jazba ni sehemu ya madhaifu yake
-----Jambo pekee litaleta mabadiliko ya kweli katika taifa hili ni KATIBA na katika hilo mr president yupo kimya na ccm yake
-----Kwa sheria hizi mbovu na utaratibu huu mbovu wa uendeshaji wa serikali,tutajikuta tunalipa fidia kubwa sana kutokana na maamuzi ya mr president,hata ikifanya sawa ila kwa sheria hizi watatushitaki na tutalipa.
----Wahafidhina ndani ya ccm hawatakuwa tayari kuona mr pombe akigusa masilahi yao,mfano ni yale ya zanzibar na jecha salim jecha na wakubwa wenziwe.
NB-kwa jinsi hii msemo wa hapa kazi tu utapata shida katika utekelezaji wake,vinginevyo mr president namuombea kila la kheri,auvae ujasiri ili aushinde mtihani uliopo mbele yake,katiba mpya ndiyo silaha yake na tunasubiri tuone hilo na MUNGU AKUPE AFYA NJEMA UKATIMIZE MAJUKUMU YAKO VEMA;
No comments:
Post a Comment