Saturday, January 2, 2016

DOA NI DOA JAPO HUENDA SI DOA BAYA

   Kuwa na aina Fulani ya kufikiri ndiko huleta tofauti ya baadhi ya tafsiri ya mambo hapa duniani,na ni jambo la kheri na ndilo jambo linaletelezea tafrani katika dunia hii.
   Doa linakuwa ni doa kutokana na jamii Fulani ya wanyama au vitu Fulani kutokuwa na mfanano unaolingana kimantiki na kimwonekano,kwa mfano katika nguo yenye rangi nyeupe katika uhalisia wake au mchanganyiko wa rangi ulio rasmi,ikatokea rangi nyingine ikaingilia rangi hizo kwa bahati mbaya au kwa makusudi basi hilo huitwa doa.
    Pia kwa binadamu kama kunajambo ambalo limekubaliwaa na jamii iliyokubwa,likaonekana ni jambo jema, akatokea mmoja wapo akaenda kinyume na uhalisia huo,basi huyo mtu anakuwa anaitia doa jamii hiyo,si kwa sababu amekosea la hasha bali ni kwa sababu ameenda kinyume na matakwa ya walio wengi.

   Hoja yangu ni nini hapa,katika serikali inayoundwa na president Pombe yapo madoa ya wazi ambayo yanaifanya serikali yake ionekane huenda ikawa ya kawaida kama serikali nyingine zilizopita na  kufanya mambo ya hovyo,kama ikiwepo tofauti basi ni ile tofauti ya kawaida ya kibinadamu ambayo kiasili lazima itokee.
   Kwa nini naamini hivi,taifa imara huwa halitegemei mtu imara ili kutengeneza future ya taifa, bali huhitaji mfumo bora na imara ambao utatengeneza watu imara,Mr Pombe ni mtu imara ambaye hakutengenezwa na mfumo imara.kwa hiyo hata yale anayoyafanya kama rais wangu,mengi ni mambo yanayofaa,lakini anayafanya yeye kama mr pombe siyo mfumo .na hii ni hatari kwa ustawi wa taifa.
    Kuna majina ya mawaziri ambao hapo awali walihusishwa na skendo mbali mabali kubwa za kifisadi, na makatibu wakuu pia,lakini hao ha leo wameaminiwa na kupewa sehemu nyeti,huenda walikiri dhambi zao na wakasamehewa hilo halijulikani, na mfumo wetu hautoi mwanya huo.haya madoa huenda si madoa mabaya labda wasiwasi wangu tu.lakini yananifanya nitazame upya dhamiri ya kuivaa nguo hii kwa mara ya pili.
   Kama mambo ya taifa yataendeshwa kwa utashi wa viongozi na si kwa mujibu wa sharia mama ambayo ni katiba,basi madoa haya yatakuwa ni madoa halisi,kama matendo ya waziri mkuu Mr Majaliwa na Mr Pombe yakiwa yanatoka mioyoni mwao kweli,basi waweke misingi hiyo kikatiba,watanzania walishatoa maoni yao lakini yalikataliwa na ccm kwa maneno na vitendo,lakini ccm ni chama cha siasa kama vyama vingine hakina mamlaka ya kukanyaga maoni ya raia,japo hili lipo kikatiba mpaka leo lakini ibara hii ilivunjwa na ccm kwa makusudi kwa malengo yao hasi juu ya taifa hili.
anilunya

    Mfano Mh Rais  ameteua mawaziri nje ya wabune wa majimbo ambao wapo kikatiba hii inadhihirisha kwamba hoja ya kutenganisha ubunge na uwaziri ni hoja ambayo inaishi vichwani mwao,ila hawataki tu,wizi wa kutisha bandarini,mabehewa feki na mengineyo, yanatimiliza kusudi la kuwa na mfumo bora ambao utazalisha viongozi waadilifu aina ya Magufuri.

    Mwisho huenda madoa haya yakageuka kuwa urembo katika nguo kwa muda, ila mmiliki wa nguo hii akibadilika bado haya yatakuwa madoa yaliyokubuhu,yes!

No comments:

Post a Comment