Sunday, January 3, 2016

UKISHANGAA YA MAKONGORO MAHANGA UTAAMINI YA KUSADIKIKA.

Ndugu!
     Imekuwa ni kawaida kwa binadamu kuwa na mitazamo tofauti na hiyo ndiyo imeleta maana halisi ya neno maisha.bado tu mawazo yetu hayatoki sana katika siasa maana siasa ni maisha yetu ya kila siku,na siasa hii tunayoisema ndo inaamua baadaye yako.
      Huko mitandaoni kuna andiko la ndugu makongoro mahanga ambalo kihalisia ameweka mawazo yake huru juu ya ukubwa wa serikali ya mr pombe,kwamba baada ya kupunguza idadi ya wizara basi matarajio ilikuwa ni kuona idadi ya makatibu wakuu inaendana na wizara husika,lakini  hilo limekuwa tofauti wizara moja imepewa makatibu wakuu mpaka watatu,sawa kuna hoja ya msingi kuwa lazima kuwe na watu maalum ili utendaji uende kwa kasi zaidi,lakini si hoja ya udogo wa baraza au serikali yake.
Prof.Magembe --waziri wa maliasili na utalii
     Kakituko kenyewe ambako kanachekesha kidogo na huenda ikawa imevunja record ya dunia  kuwa na makatibu wakuu wawili na naibu katibu mmoja,haijaeleweka utendaji kazi wa hawa watu utakuwaje,nani hasa atakuwa msemaji wa mwisho juu ya naibu katibu huyu,sawa,huenda mawazo ya rais ni makubwa kuliko yangu,lakini bado haki ya kuhoji hili na kupatiwa jibu sahihi ni mhimu,
     Nadhani kungekuwa na katibu mkuu mmoja katika kila wizara kuendana ya idadi ya wizara,alafu kuwe na idara nyigi zenye wakurugenzi wenye taaluma husika ambao watafanya kazi chini ya katibu mkuu ambaye atakuwa oversee wa idara zote.hapo dhana ya ujenzi au uundwaji wa serikali ndogo ingeleta maana kubwa zaidi.
      Ukishangaa ya makongoro utaamini ya kusadikika,kushauri ni jambo moja kufanyia kazi ushauri ni jambo lingine hasa ukijaribu kushauri kwenye jambo litakalo kosoa maamuzi yake kiafrika hili ni jambo gumu mno.
          siku njema na asante kwa kusoma ujumbe huu

No comments:

Post a Comment