Huenda ikawa ni bahati kuliko neno bahati lenyewe unavyoweza kulitamka ni ile zawadi ya kuiona leo tena,wengi walitamani lakini hawajachaguliwa,tuliochaguliwa tunayo kila sababu ya kumshukuru mungu na kumrudishia sifa na utukufu yeye,maana si kwamba ni watakatifu sana bali mungu analo kusudi na wewe......MWAMBIE KITU MUNGU WAKO LEO
Kila uchwao tumekuwa na malalamiko ya kila aina hasa katika utendaji wa serikali na watu binafsi,je malalamiko haya mwisho wake ni lini?na kwa nini kila siku utendaji kazi wetu ni wa kivivu mmo,utakuta kuna sababu za msingi na sababu za hovyo tu ambazo zinasababisha hali hii.lakini kimsingi nami nakubaliana kabisa na takwimu za serikali yenyewe, ambazo zimetolewa jana na mh jenista mhagama waziri wa kazi,vijana,sera na uratibu wa bunge kutoka ofisi ya waziri mkuu,,kwamba asilimia 71 ya watanzania wote wanakaa vijiweni au kwa lugha ya staha wanafanya mambo ambayo si ya uzalishaji.
Kama asilimia 71 inafanya mambo ya hovyo na kwa mujibu wa sensa ya 2012 inaonyesha zaid ya asilimia 67 ya raia wa tanzania ni vijana ambao hasa ndiyo nguvu kazi ya taifa.maana yake nini karibu robo tatu ya vijana wote tanzania wanafanya mambo ya kawaida tu ambayo hayawezi kuleta matokeo chanya katika taifa,na vijana wamekubali hilo na mamlaka zimeruhusu hilo,mifumo ya elimu emeruhusu hilo na tumekosa nia ya kutokea.
Serikali iweke mifumo bora na rafiki kwa raia wake ili tuwe na vijana ambao ni productive kutoka ndani ya mioyo yao,yaani wapende kufanya kazi na kazi iwe na misingi na heshima ya utu,kwa maana kuwe na mishahara inayoendana na mahitaji ya wakati,sheria za kazi zinazojali haki za binadamu,lakini pia kwa asilimia kubwa watu hawa wanapenda kujiajiri katika kilimo na viwanda vidogo vidogo, ni jukumu la serikali kuwawekea mazingira rafiki na tasisi za fedha,pia uhakika wa masoko,miundo mbinu na zaidi kupewa mafunzo ya mara kwa mara kutoka kwa wadau wa ndani na nje,,,hapo tutaweza kuongeza kiwango cha vijana wanaopenda kufanya kazi bila shuruti.
Mh.rais amesema vijana watoke katika vijiwe vya pool na kwenda kulima kwa hiyari au kwa nguvu.ni kauli ya kishujaa sana kutoka kwa rais wangu,lakini utekelezaji wake unahitaji maarifa na ushirikiano wa tasisi mbali mbali kwa maana nyingine hili ni jambo mtambuka,migogoro ya ardhi,vyama vya ushirika,uhakika wa maji,miundo mbinu,viwanda na biashara,na utafiti wa kina kwa kila aina ya mazao uwe wazi na upelekwe mashambaji siyo mjini kama ilivyo sasa,pia viongozi wenyewe wawe mfano chanya ili kila mlipa kodi aone kodi yake inalidaidia taiafa na kuwalipa watumishi wenye tija kwa taifa na si vinginevyo.
![]() |
NA WABUNGE NA POLISI WAMO |
![]() |
PAMOJA NA HALI KUWA TETE BADO WANAPENDA POOL |
No comments:
Post a Comment