Kuna kila sababu ya kutakiana kila lililo la kheri mwaka huu mpya unaoanza soon...
OMBI Langu kwenu-----kama kuna jambo ulikosea 2013 usijilaumu sana ila usirudie tena kutenda hilo jambo maana mungu amekupitisha hapo kwa makusudi yake....
Tuesday, December 31, 2013
Saturday, December 28, 2013
ABARIKIWE YULE ALIYENIPA KIBALI CHA KUIONA TENA LEO NA KUIFANYA ALBAM HII IWE OK.
Namshukuru sana mungu kwa wema wake kwa kuniwezesha kumaliza albamu hii ambayo imejaa injili ya kweli ya bwana wetu yesu kristo.hakikisha unajipatia nakala yako very soon,,lakini pia kwa wale ambao wanaweza kufikia mitandao ya kijamii basi ingia hulkshare utasikiliza nyimbo zote na ukitaka pakua ukawabariki na wengine nyumbani....maana tumepewa bure nasi pia yatupasa tutoe bure.....SIKU YA HUKUMU TUSIJE TUKAHUKUMIWA KWA HILO NA SOON YOUTUBE VIDEO ZITAKUWA OK
Friday, December 27, 2013
WATU WANAZIDI KUBUNI VITU HII NI MELI AMBAYO ITAKUWA MJI MKUBWA UNAOELEAA MAJINI
Hii ni moja kati ya mwonekano wa meli hiyo ambayo itakuwa na kila kitu ambacho kinapatikana katika mji wowote ulioendelea.
Ni kazi hasa wabunifu wetu mpo wapi...acheni kutujengea majengo kama ya kaliakoo ambayo ni hatari kwa maisha yetu.....
Thursday, December 26, 2013
TANZANIA NA RECORD YA POMBE NA MAGONJWA
Taifa langu la tanzania nalipenda na nitaendelea kulipenda japo kunachangamoto ambazo hatuwezi kuzikwepa lazima tuzizungumze tena kwa uwazi kabisa ili wadau wenye dhamana wafanye yawapasayo.
Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa mataifa TANZANIA ni NCHI ya tatu afrika kuwa na walevi au wanywa pombe wengi ikiwa nyuma ya UGANDA na NAIGERIA inayoongoza,lakini katika takwimu hizo 86% ya walevi hawa wanakunywa pombe chafu yaani zile ambazo hazijathibitishwa na mashirika ya viwango ni hatari,10% wanakunywa vilevi vilivyopimwa na 4% wanakunywa vilevi vikali kutoka nje.....
Vile vile tunashika nafasi ya 5 kuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi duniani.nyuma ya AFRIKA KUSINI,.NAIGERIA,INDIA,KENYA, hii ni hatari sana kwa ustawi wa taifa na uchumi wetu....TUBADILIKE

HII NI KARNE AMBAYO UTANDAWAZI UNAINGIA KWA KASI YA AJABU,PENI INAYOPIGA PICHA
Katika hali ambayo inaonekana kama maendeleo ya haraka katika tekinolojia ya habari na mawasiliano ni pamoja na hizi aina ya peni ambazo zinauwezo wa kupiga picha kwa ubora wa hali ya juu pamoja na kupata sauti yenye ubora wa kutosha,,,,,Haya sasa wandishi wa habari za uchunguzi uwanja ni wenu,msije mkatoa sababu ambazo zitakuwa hazina mashikoooooo.

Thursday, December 19, 2013
BUNGE LETU LA TANZANIA LINAPOGEUKA KIJIWE CHA STORY ZA NYUMBA NDOGO!!
Habari zenu ndugu zanguni,,
Nashukuru sana mwenyezi mungu kwa kunipa uwezo wa kuiona leo na akanipa pia wasaa wa kuandika taarifa hii kwa ufupi sana,bunge letu la tanzania limezidi kuwa na vituko lakini kwa kituko hiki, hapana lazima tuweke sawa.
Kuna mbunge mmoja anaitwa mr nchemba pale bungeni kamwambia mwenzake mr mbowe kwamba anatumia madaraka vibaya na kimada ambaye pia ni mbuge wa viti maaluma chadema.sina tatizo na taarifa yake wala siyo jambo zuri kuwa na kitu alafu unakisema kwa mafumbo mafumbo huo huitwa unafiki,kwa hiyo kwa hilo bwana mwigulu, mimi binafsi nakupongeza kwa kuacha kuwa mnafiki.
Ila shaka yangu ni kwamba kama siasa yetu imefika hapa basi hatapona mtu maana asilimia kubwa ya wakubwa wetu hawa wanaongoza kuwa na nyumba ndogo au vimada,kwa hiyo mtu yeyote ambaye anataka kulisema hili lazima kwanza ajihoji mwenyewe usafi wake ndipo aende kwa jirani yake.
Lakini pia kuacha kujadili mambo ya msingi yanalolihusu taifa na kujadili mtu na maisha yake hili nalo ni upungufu kwa siasa zetu za tanzania maana tangu ngazi ya juu tungesema mwenyezi mungu aweke wazi yale yanayotendeka ,basi hata angepatikana kiongozi mmoja au wawili tu waadilifu na ndoa zao..KWA KIFUPI HAKUNA MWENYE UBAVU WA KUMSEMA MWENZIE KWA TABIA ZAO HILI NI JAMBO AMBALO LAZIMA MJIREKEBISHE;;;;

Subscribe to:
Posts (Atom)