Kuwa na aina Fulani ya kufikiri ndiko huleta
tofauti ya baadhi ya tafsiri ya mambo hapa duniani,na ni jambo la kheri na
ndilo jambo linaletelezea tafrani katika dunia hii.
Doa linakuwa ni doa kutokana na jamii Fulani
ya wanyama au vitu Fulani kutokuwa na mfanano unaolingana kimantiki na
kimwonekano,kwa mfano katika nguo yenye rangi nyeupe katika uhalisia wake au
mchanganyiko wa rangi ulio rasmi,ikatokea rangi nyingine ikaingilia rangi hizo
kwa bahati mbaya au kwa makusudi basi hilo huitwa doa.
Pia kwa binadamu kama kunajambo ambalo
limekubaliwaa na jamii iliyokubwa,likaonekana ni jambo jema, akatokea mmoja
wapo akaenda kinyume na uhalisia huo,basi huyo mtu anakuwa anaitia doa jamii
hiyo,si kwa sababu amekosea la hasha bali ni kwa sababu ameenda kinyume na
matakwa ya walio wengi.
Hoja yangu ni nini hapa,katika serikali
inayoundwa na president Pombe yapo madoa ya wazi ambayo yanaifanya serikali
yake ionekane huenda ikawa ya kawaida kama serikali nyingine zilizopita na kufanya mambo ya hovyo,kama ikiwepo tofauti
basi ni ile tofauti ya kawaida ya kibinadamu ambayo kiasili lazima itokee.
Kwa nini naamini hivi,taifa imara huwa
halitegemei mtu imara ili kutengeneza future ya taifa, bali huhitaji mfumo bora
na imara ambao utatengeneza watu imara,Mr Pombe ni mtu imara ambaye
hakutengenezwa na mfumo imara.kwa hiyo hata yale anayoyafanya kama rais
wangu,mengi ni mambo yanayofaa,lakini anayafanya yeye kama mr pombe siyo mfumo
.na hii ni hatari kwa ustawi wa taifa.
Kuna majina ya mawaziri ambao hapo awali
walihusishwa na skendo mbali mabali kubwa za kifisadi, na makatibu wakuu pia,lakini
hao ha leo wameaminiwa na kupewa sehemu nyeti,huenda walikiri dhambi zao na
wakasamehewa hilo halijulikani, na mfumo wetu hautoi mwanya huo.haya madoa
huenda si madoa mabaya labda wasiwasi wangu tu.lakini yananifanya nitazame upya
dhamiri ya kuivaa nguo hii kwa mara ya pili.
Kama mambo ya taifa yataendeshwa kwa utashi
wa viongozi na si kwa mujibu wa sharia mama ambayo ni katiba,basi madoa haya
yatakuwa ni madoa halisi,kama matendo ya waziri mkuu Mr Majaliwa na Mr Pombe
yakiwa yanatoka mioyoni mwao kweli,basi waweke misingi hiyo kikatiba,watanzania
walishatoa maoni yao lakini yalikataliwa na ccm kwa maneno na vitendo,lakini
ccm ni chama cha siasa kama vyama vingine hakina mamlaka ya kukanyaga maoni ya
raia,japo hili lipo kikatiba mpaka leo lakini ibara hii ilivunjwa na ccm kwa
makusudi kwa malengo yao hasi juu ya taifa hili.
Mfano Mh Rais ameteua mawaziri nje ya wabune wa majimbo
ambao wapo kikatiba hii inadhihirisha kwamba hoja ya kutenganisha ubunge na uwaziri
ni hoja ambayo inaishi vichwani mwao,ila hawataki tu,wizi wa kutisha
bandarini,mabehewa feki na mengineyo, yanatimiliza kusudi la kuwa na mfumo bora
ambao utazalisha viongozi waadilifu aina ya Magufuri.
Mwisho huenda madoa haya yakageuka kuwa
urembo katika nguo kwa muda, ila mmiliki wa nguo hii akibadilika bado haya
yatakuwa madoa yaliyokubuhu,yes!