Friday, April 15, 2016

NINI SABABU YA ONGEZEKO LA VIJANA MIJINI?

Salama ndugu zangu!
                Na Alex Nyaganilwa
    Hakuna siku ambayo itapita bila kumshukuru mungu,maana yeye ndiye mwenye kila aina ya uwezo mkubwa unaozungumzwa na binadamu,pekee anayestahili kuabudiwa na kutukuzwa....endelea

    Ongezeko la vijana mijini afrika si jambo geni sana,watu wanatoka vijijini na kuja mijini wakiwa na matumaini makubwa sana juu miji hiyo,lakini pindi wafikapo mijini hali huwa tofauti sana na wachache sana ndiyo hufikia ndoto zao kwa urahisi na kwa haraka,kukiwa na sababu kadhaa.
  Laakini kwanini watu wanakimbia vijijini,sababu moja kubwa ni kwamba viongozi wa bara la afrika kiwango chao cha kuwaza ni cha kawaida sana,ndio maana wakaona ni bora waweke miundo mbinu inayowagawanya raia wake kwa umbali usiokifanika,mfano unakuta mji una wakazi zaidi ya milion mbili lakini hakuna,umeme,maji,hospitali wala shule na zaidi hata barabara zenyewe hamna..hutegemei kijana wa dotcom abaki hapo kama zuzu,lazima atoke.

  Anatoka anaenda wapi?anakuja mjini ambako nako hakuna mipango miji,mtu popote anaweka kibanda analala,akiamka atakuwa machinga au atauza maandazi na pipi barabarani na maisha yake yataenda murua kabisa, maana yeye anachojua siku yake ya leo tu,kesho ni ya mungu.na saerikali zipo na zinafanya kazi,lakini kazi zao ni za kawaida si kazi za kutumia akili nyingi kama wengine duniani wafanyavyo.

  Kufikia mwaka 2050 afrika pekee itakuwa na vijana bilioni moja watakao kuwa mijini,utake usitake,wanakuja kutafuta maisha na ni haki yao kwa mujibu wa katiba,lakini pia hata nature ya uumbaji haibagui mtu kuishi popote,unaweza kuishi popote,lakini wenzetu duniani huko wamejitahidi kuweka utaratibu mzuri unaozingatia utu wa mwanadamu,ukiwa unataka kutoka sehemu moja kwenda nyingine ufuate utaratibu huo,na si kufuta mahitaji mhimu,wao wameweka mahitaji mhimu karibu mahala pote wanapoisha raia wao,maana yake nini,wao wanajua mipango miji na wanajua kasi ya ongezeko la raia wao na wanajiandaa kukabiliana nalo.

  Afrika kila jiji lina matatizo yake yanafanana.ama siku zote miundo mbinu yetu haitoshi,ujenzi holela utadhani vichaa hatupendi vitu vizuri, utadhani hatuna macho ya kuona kwamba watu wanaongezeka,ama tu serikali na viongozi walio wengi ni wezi wa mali za umma kama wao wataishi mbinguni siku zijazo,hili ni bomu amabalo litalipuka muda si mrefu na halitaacha mtu nyuma wote tutaathirika na bomu hili kwa namna moja ama nyingine.

  Ongzeko la watu linapozidi kuwa kubwa bila mipango miji,athali zake ni nyingi,magojwa ya kuambukiza,uharifu uliopitiliza,vikundi vya kigaidi,rushwa mbali mbali na zaidi vita,,,watu wakikosa mahitaji mhimu na wakiona wachache wanapata na wao hawapati lazima wadai kwa nguvu na serikali haitakubali ndio maana tunaona afrika vita za wenyewe kwa wenyewe ni nyingi sababu moja wapo ni hii ya viongozi kukosa mtazamo chanya kwa raia wake,

  Nini kifanyike,mfano kwa nchi yangu tanzania,hakuna muujiza utakuja lazima tuanze mwanzo mpya,tushirikishe watalamu na wanasiasa tupate sera bora ya makazi,ili tuanze kuweka makazi bora kila sehemu walipo wananchi ,serikali iweke mipango rafiki ya kufikisha huduma mhimu pande zote za nchi yetu ili tupunguze ongezeko la vijana mijini.nafahamu miaka mitano au kumi haitoshi kuona matokeo ya mipango bora,basi kama ni hivyo tuweke dira bora ya taifa letu,,,,,asante kwa kusoma
     

UVIVU NI JANGA LA TAIFA ,SIYO POOLTABLE TU

Habari ndugu zangu,

  Huenda ikawa ni bahati kuliko neno bahati lenyewe unavyoweza kulitamka ni ile zawadi ya kuiona leo tena,wengi walitamani lakini hawajachaguliwa,tuliochaguliwa tunayo kila sababu ya kumshukuru mungu na kumrudishia sifa na utukufu yeye,maana si kwamba ni watakatifu sana bali mungu analo kusudi na wewe......MWAMBIE KITU MUNGU WAKO LEO

  Kila uchwao tumekuwa na malalamiko ya kila aina hasa katika utendaji wa serikali na watu binafsi,je malalamiko haya mwisho wake ni lini?na kwa nini kila siku utendaji kazi wetu ni wa kivivu mmo,utakuta kuna sababu za msingi na sababu za hovyo tu ambazo zinasababisha hali hii.lakini kimsingi nami nakubaliana kabisa na takwimu za serikali yenyewe, ambazo zimetolewa jana na mh jenista mhagama waziri wa kazi,vijana,sera na uratibu wa bunge kutoka ofisi ya waziri mkuu,,kwamba asilimia 71 ya watanzania wote wanakaa vijiweni au kwa lugha ya staha wanafanya mambo ambayo si ya uzalishaji.

  Kama asilimia 71 inafanya mambo ya hovyo na kwa mujibu wa sensa ya 2012 inaonyesha zaid ya asilimia 67 ya raia wa tanzania ni vijana ambao hasa ndiyo nguvu kazi ya taifa.maana yake nini karibu robo tatu ya vijana wote tanzania wanafanya mambo ya kawaida tu ambayo hayawezi kuleta matokeo chanya katika taifa,na vijana wamekubali hilo na mamlaka zimeruhusu hilo,mifumo ya elimu emeruhusu hilo na tumekosa nia ya kutokea.

  Serikali iweke mifumo bora na rafiki kwa raia wake ili tuwe na vijana ambao ni productive kutoka ndani ya mioyo yao,yaani wapende kufanya kazi na kazi iwe na misingi na heshima ya utu,kwa maana kuwe na mishahara inayoendana na mahitaji ya wakati,sheria za kazi zinazojali haki za binadamu,lakini pia kwa asilimia kubwa watu hawa wanapenda kujiajiri katika kilimo na viwanda vidogo vidogo, ni jukumu la serikali kuwawekea mazingira rafiki na tasisi za fedha,pia uhakika wa masoko,miundo mbinu na zaidi kupewa mafunzo ya mara kwa mara kutoka kwa wadau wa ndani na nje,,,hapo tutaweza kuongeza kiwango cha vijana wanaopenda kufanya kazi bila shuruti.

 Mh.rais amesema vijana watoke katika vijiwe vya pool na kwenda kulima kwa hiyari au kwa nguvu.ni kauli ya kishujaa sana kutoka kwa rais wangu,lakini utekelezaji wake unahitaji maarifa na ushirikiano wa tasisi mbali mbali kwa maana nyingine  hili ni jambo mtambuka,migogoro ya ardhi,vyama vya ushirika,uhakika wa maji,miundo mbinu,viwanda na biashara,na utafiti wa kina kwa kila aina ya mazao uwe wazi na upelekwe mashambaji siyo mjini kama ilivyo sasa,pia viongozi wenyewe wawe mfano chanya ili kila mlipa kodi aone kodi yake inalidaidia taiafa na kuwalipa watumishi wenye tija kwa taifa na si vinginevyo.

NA WABUNGE NA POLISI WAMO
  Uzalendo hausemwi tu na kuishia majukwani, huwezi ona matokeo ya uzalendo kwa kusema kwa maneno,lazima vitendo chanya vitamalaki katika kila idara ya serikali,kwa viongozi wa ngazi zote wa kuteuliwa au kuchaguliwa waoneshe uzalendo kwa vitendo,ndipo watanzania wataanza kufanya kazi baada ya kuona wakubwa wao wakiwa mifano chanya ya kuigwa.hakuna njia ya mkato katika kukuza uzalendo wa watu kulijenga taifa lao lazima tuwe na mkakati wa kitaifa.na huu hatakwepwa kirahisi, mtajaribu leo kama watawala kuiacha misingi ya uzalendo katika kitabu cha makubaliano cha taifa(katiba)ili mtimize malengo yenu,mtafanikiwa kwa sababu mnayo dola,ila uzalendo bado utaendelea kusuburi misingi yake mpaka itakapo kuja na haijulikani ni lini, ila mimi ninayo imani, ipo siku misingi ya uzalendo itakuja kuwekwa katika katiba na kiongozi mzalendo atakayechoshwa na haya,ipo.

PAMOJA NA HALI KUWA TETE BADO WANAPENDA POOL
  Mtanzania mmoja mmoja amka tumia uwezo wako aliokupa mwenyezi mungu kupambana na mazingira yako,katika taifa letu kila mtu aliyepo mbele yako ni adui,wavivu,waongo,wanafiki na hupenda kuuliza badala ya kuulizwa,sifa ya kuulizwa lazima uwe na ubongo huru unaofikiri mambo huru wakati wote,kwa maana nyingine jitafutie maarifa popote kwa nguvu na jitihada za kutosha..utafanikiwa......."IKIWA MWINGINE ANAFANYA,KWA NINI AKILI YANGU ISHINWE KUFANYA JAMBO LINGINE TOFAUTI NA HILO"

Wednesday, April 13, 2016

INUA UELEWA WAKO KWA KIJIFUNZA KWA WENGINE

INUA UELEWA WAKO KWA KIJIFUNZA KWA WENGINE


Salama ndugu zangu!!
   Napenda kumshukuru Mungu mwenyezi aliyetupa nafasi ya kuiona leo,pia kuwapa pole ndugu zangu wote walio katika mateso ya dunia hii,lakini jipe moyo maana mtetezi wako yuu hai na uamzi upo juu yako leo….endelea

  Inua uelewa wako kwa kujifunza kutoka kwa wengine,ni sentensi ndefu pia yenye maana kubwa sana na urefu wenye sawia na urefu wake,pia inatafsiri uhalisia wa maisha ya binadamu ya kila siku.kujifunza kumegawanyika katika makundi mawili katika mantiki yake,na wote hapa dunia tupo katika moja ya makundi haya.

-KUJIFUNZA MAMBO CHANYA-kila binadamu aliyepewa nafasi ya kuishi anacho cha kujifunza kutoka kwa binadamu mwingine kwa lugha nyepesa tunaweza sema kila binadamu ni mwalimu wa mwenzake katika upande Fulani wa ubobevu wake katika ubongo wake.wapo watu ambao huona aibu kujinza kwa sababu wanaona aibu?yaani unayakosa maarifa chanya kwa sababu tu Fulani atanicheka au Fulani akijua atatusumbua sana kwa hiyo hutaki kutoa maarifa hayo kwa wengine kwa sababu tu utasumbuliwa kufanikiwa kwa mwingine???!hizi ndizo kesi nyingi sana katika bara letu la afrika.lakini nikutie moyo “mtu yoyote anayefikiri chanya hutenda mambo chanya”vitu vyote unavyotumia gharama kubwa kuvipata na muda mwingine vinakamilisha furaha yako, vilibuniwa na watu wanaofikiri chanya na wanaopenda kujifunza bila mipaka,kwa hiyo kama akili yako unataka ifurahie kujifunza basi anza leo “kuheshimu mawazo na vipaji vya wengine”
  Hakuna uchaguzi wenye njia moja,kila uchanguzi una machaguo zaidi ya moja, hii yote ni kipimo cha kujua ni nani hasa anajua uwezo wa akili yake na vipawa vyake tangu kuumbwa kwake,ili uchochee kipawa chako lazima ujifunze mambo chanya kwa upande huu wenye mawazo chanya,
  Unaweza kujifunza kwa njia nyingi lakini njia bora zaidi ni ile ya kusikia sauti yako ya ndani inakwambia nini na matokeo ya sauti hiyo igeuze katika vitendo na watu wakuzungukao watasema wewe si wa kawaida..kuwa mpole kiasi,yape masikio nafasi kubwa kuliko mdomo wako, kisha pongeza panapofaa kupongeza na pia toa maoni yanayofaa kwa uwazi pale inapotakiwa ,,hatimaye utakuwa mtu bora na jamii yako itasema huyu mtu si wakawaida na kwa matokeo ya mawazo yako hata baada ya kuondoka mwili wako hapa duniani bado athali zako chanya zitaishi,

 KUJIFUNZA MAMBO HASI-Mambo yote hasi ndio chanzo cha mateso na mahangaiko ya wanadamu hapa duniani,kwa hiyo kama unatenda jambo hasi mahala ulipo basi ujue kwamba kama siyo leo kwa mawazo yako na matendo yako ipo siku binadamu mwingine atapata matokeo hasi kutokana na maisha yako.
  Asilimia kubwa vitu vyote vyenye chembe ya uhasi ndani yake ndivyo vinatazamwa na kuwekwa katika vyombo vya habari,magazeti,mitandandaoni na kwingineko,lakini nini sababu?sababu kubwa binadamu wengi wanafurahia majibu ya kawaida ya maswali yao bila kuuliza maswalimhimu ya nyongeza,na watengenezaji wa mambo hayo hawajatoa nafasi ya maulizo kwa bidhaa zao au huduma zao zinazodhorotesha kiwango cha kufikiri cha mwanadamu,na afrika sisi ndio wahanga wa tatizo hili.kama hawataki kuulizwa basi kabla ya kununua huduma yake au bidhaa yake jiridhishe kwanza mwenyewe kwa masilahi yako na kizazi chako.
  Ikiwa  una uwezo wa kuuliza maswali mhimu katika kila hatua ya maisha yako,iko siku utapata jibu sahihi na litakupelekea kufanya jambo chanya.”hakuna dunia majibu sahihi ya mahitaji yako mpaka utakapojua wewe unahitaji nini”kwa hiyo kuanzia leo usiwaze hasi,maneno kama siwezi,sijui,hajui,labda Fulani,nitafanya kesho,sina uhakika, ni maneno yanayopelekea binadamu uwaze hasi,epukana nayo leo ili uipe nafasi akili yako  kujifunza.
 
  Hakuna namna bora katika kujiletea maendeleo katika dunia isiyo na huruma kama hii, lazima ufungue kurasa mpya katika ubongo wako, uwaze na kujifunza mambo chanya kutoka kwa binadamu wenzako na kutoka mawazo binafsi yanayoletwa na Mungu wako kukabili mazingira yako.na hayo ndiyo mawazo bora zaidi kupata kutokea maa
na ndiyo matokeo ya bidhaa na huduma zote hizi duniani,,,WEWE UNAWEZA ANZA LEO

  

Tuesday, April 12, 2016

NINI MAANA YA WAKATI WA MAAMUZI MAGUMU

salama ndugu zangu!!!!
  Tumaini langu ni kubwa kwa mungu wetu aliyetupa tena nafasi ya kuiona leo,nasema asante hata kwa niaba ya msomaji wangu huyu,ambaye labda alisahau kukuambia asante nyakati za asubuhi.endelea......
      
       "Moja kati ya sifa mhimu ya kiongozi ni kufanya maamuzi magumu,i hali anazo taarifa nyingi mkononi zenye maoni yanayokinzana"moja ya kipimo ukitaka kujua kiongozi bora..

Leo nimeona tuzungumze jambo moja mhimu sana katika maisha yetu ya kila siku,na jambo lenyewe ni maamuzi,watu wengi tumekuwa tukichelewa kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yetu kutokana  tu na hofu ya mabadiliko,lakini ukishafanya maamuzi, majuto yanageuka na kujilaumu kwanini ulichelewa kufanya maamuzi mapema maana ulipo baada ya maamuzi yako ni bora zaidi.

  Kila aina ya maamuzi yana ghalama zake ambazo lazima zibebwe ama na mfanya maamuzi,au mtu wa pili na  wa tatu.lakini kitu kinachobeba msingi wa maamuzi ni kusudi la kufikia matokeo chanya yenye tija kwa jamii kubwa zaidi,hii imepelekea wengine kushindwa kuendana au kuzikabili gharama hizo za maamuzi ambazo zimegawanyika katika makundi kadhaa,moja mali au fedha,hisia(msongo wa mawazo) upweke,aibu,n.k...lakini hakuna maendeleo yaliyokuja bila kufanya maamuzi yanayokinzana na walio wengi ambao kikawaida hufikiri kawaida,kwa jinsi hiyo popote ulipo wewe ni kiongozi wa akili yako na jamii ingine ama familia na kuendelea, basi ni wasaa wako wa kufanya maamuzi sahihi yatakayo chora dira ya kizazi chako.

 Lakini pia kiongozi bora hufanya tathimini ya maamuzi yake na kupokea matokeo yake na kuyabeba mwenyewe bila kusaidiwa na awaye,kama alifanya makosa basi lazima awe tayari kulikabili hilo na kuona namna bora zaidi ya kusonga mbele.
  viongozi wengi wa afrika  wameleta homa ya afrika,hawafanyi maamuzi yenye tija kwa mataifa yao na hii imepelekea raia wake kuzoea njia za mkato, na wakati wachache wakifanya maamuzi sahihi huonekana wamekosea na hukemewa hadharani hii haikubaliki popote duniani,lazima tubadilike kabla ya kusema fikiri nini unataka kusema na kwa nini unasema na je ni mahala sahihi lakini la zaidi je ni muda sahihi?

Usisite kufanya maamuzi magumu hata kama unazotaarifa nyingi mkononi mwako,wewe kama kiongozi kitu cha kufikiri ni maslahi mapana ya jamii yako,na
uwe tayari kupokea mawazo tofauti na maamuzi yako,na kauli thabiti huwa ni kupokea mawazo na kuyapima katika mizania inayofaa na ikiwa inafaa itatumika siku za usoni bila kubatilisha maamuzi ya awali...huyu hupimwa kama kiongozi imara na shupavu mwenye uwezo wa kusimamia maamuzi yake.ni wachache duniani....ukianza leo utakuwa miongoni mwa wale wachache.

Monday, April 11, 2016

NJIA SITA ZA KUJENGA TEAM YA USHINDI ILI KUFIKIA MALENGO CHANYA KATIKA BIASHARA AU HUDUMA

Salama ndugu zangu!
  Tazama mbinu sita za kukuwezesha kufikia malengo chanya katika huduma au biashara yako,hili limekuwa ni tatizo kubwa sana katika bara letu la afrika watu wake hatuwezi kufanya biashara kwa ufanisi kutokana na uelewa mdogo wa kudeal na biashara hizo,
  Afrika ndiyo bara pekee duniani ambalo malighafi bado inapatikana kwa wingi na inailisha dunia nzima,ila watu wake ni masikini wa kupigiwa mfano duniani,hili ni jambo la kulipiga vita mchana na usiku,tuongeze bidii ya kujifunza kila siku ili nasi tuwe katika ushindani huu.

1-NGUVU NA AKILI ELEKEZA KUPATA UONGOZI MADHUBUTI-uongozi mbovu huzalisha team mbovu na uongozi bora na imara huzalisha team bora na imara,ukiwa na uongozi wa kupigiwa mfano utakuwa na team yenye maadili,sikivu,na yenye ari ya kushinda muda wote,maana kiongozi wao ni mfano chanya katika maisha yao ya kazi na nje ya kazi,kwa hiyo kitu cha kwanza ni uongozi bora na imara.

2-WEKA MALENGO CHANYA KWA UWAZI-ili team yako ilete matokeo chanya lazima watu wote wajue nini hasa dira na wapi mnataka kufika kwa pamoja,kukiwa na uwazi katika malengo yenu itapelekea kuwe na utekelezaji wenye tija na unaojali ushindani wa soko,lakini pia utekelezaji unaojali muda na thamani na ubora wa  huduma au bidhaa husika,uwajibikaji na moyo wa kizalendo si kitu hutokea tu bali hujengwa kwa misingi ya utu na heshima.

3-ELEZA NA IFAHAMIKE KWA UFASAHA MISINGI,SHERIA,KANUNI NA TARATIBU -ili uwe na matokeo chanya katika mchezo wowowte lazima kuwe na sheria na taratibu zake, na haijalishi sheria zipo,je sheria hizo zinafahamika na zipo katika misingi ya utu?watu wengi hatupendi sheria,lakini lazima team yako ielezwe umhimu wa kuwa na taratibu hizo na mmoja mmoja ajua mantiki ya kila taratibu,hapo italeta kujua mipaka ya kila mtu na kuiheshimu kwa hiyari.

4-BUNI NA KUKUZA MBINU MPYA KATIKA UTENDAJI WENU WA KAZI-hata uwe na watu wasikivu,wabunifu,na wenye furaha kazini kama mipango yenu haitaenda katika vitendo ni kazi bure,na uzuri wa utendaji umewekewa misingi yake ambayo iko wazi kabisa,kila mmoja wetu akiifuta basi tatizo tutalimaliza kwa haraka.NANI anafanya NINI  na LINI,,ukisimama katika misingi hii lazima utoboe.

5-WEKA UTAYARI KUKABILI HASARA-ukiwa na uongozi bora na watu makini wenye furaha kazini,lazima uruhusu jambo moja mhimu ambalo wengi hulikimbia,ruhusu team yako itoke na vitu vipya vya kibunifu ambayo kimsingi vina gharama za ziada ambazo huitwa hasara.lakini bila kuwa na ubunifu pia utashindwa kushindana vizuri katika ulimwengu wa soko wenye kila aina ya ubunifu.

6-SHIRIKISHA TEAM YAKO KATIKA KILA HATUA MUHIMU-team ya ushindi inakamilika ikiwa kila mmoja anakubalika na mwana team mwenzake kwa uwezo wake na wanaheshimiana kwa uwezo wao,ili uone matokeo chanya 100%lazima pia kuwe na kuheshimiana na kuthaminiana miongoni mwa wanateam kwa kiwango 100%,hii ni kazi ya kiongozi madhubuti na mwenye dira chanya ya maendeleo.daima moyo wao utakuwa mmoja, kushindwa kwa mmoja ni kushindwa kwa team nzima...
  

Asante kwa kusoma share na wengine ili tuwe na taifa la vijana wenye kuthubutu,tupeleke taifa letu mbele na tujisikie vema kutimiza wajibu wetu na kutafuta haki zetu za msingi kwa wakati.
   MUNGU AKUBARIKI SANA WEWE NA UZAO WAKO