Thursday, June 26, 2014

DINI INAPOCHUKUA UHURU WA MTU KWA 100% NI HATARI.

Ndugu zangu! 
     Kuna jambo ambalo linaendelea kwa majirani zetu hapa sudani ni jambo ambalo limeteka vyombo vingi vya habari duniani, 
     Na jambo lenyewe ni la huyu dada ambaye amezaliwa na mama mkristo na baba muislam mwenye asili ya sudani na mama mwenye asili ya ethiopia.
   Amekuwa makubwa akaamua kufanya maamuzi yake mwenyewe ya kuwa mkristo na kufunga ndoa na huyu jamaa raia wa marekani mwenye asili ya sudani kusini ambako asilimia kubwa wa raia wake katika taifa hili changa ni wakristo na huku sudani kaskazini asilimia kubwa ni waislam na nchi yao wanaiongoza kwa sharia,

 Lakini je swali linakuja.HIVI DINI ZETU HIZI ZINAZO HAKI YA KUBEBA HAKI ZETU ZOTE NA UTU WETU???/ 

Tuesday, June 17, 2014

DHANA YA NENO UZALENDO INAPOTOSHWA KWA ULEVI WA UMAARUFU NA MADARAKA

Habari ndugu zanguni!!

   Kuna hili jambo ambalo linaimbwa kila siku katika kituo kimoja cha radio na tv hapa kwetu tanzania,juu  y NENO  UZALENDO,nimepata shida sana kuelewa ndio maana nikaamua mawazo yangu niyalete hapa ili tujadiliane kwa kina juu ya neno hili na jinsi linavyopotoshwa ama kwa makusudi ama kwa kutokujua.

    UZALENDO ni neno lenye herufi nane tu lakini likiwa limebeba maana kubwa sana katika usitawi wa binadamu na mazingira.uzalendo ni upendo wa asili usio na sababu na unatafsiliwa katika mahusiano ya baina ya binadamu na mazingira,binadamu na binadamu ,binadamu na wanyama wengine.huo ndiyo unaitwa uzalendo na uzalendo haujengwi kwa mahubili ya matamasha au kwenye nyumba za ibada au ikulu uzalendo unajengwa kwa MATENDO CHANYA kwa viumbe wanaokuzunguka.
     Nimeona picha na sauti ya moja kwa moja kutoka kwa watu wenye umaarufu katika taifa letu kutoka pale dodoma wakati wanazindua wimbo wa uzalendo.nikajiuliza uzalendo huwa unazinduliwa?na unazinduliwa na watu maarufu!! kwa kucheza na kuimba ngonjera na nyimbo na kula pamoja ikulu,....
       Ukimwalika masikini asiye na uwezo wa kupata hata mlo wa siku moja na utakuwa umejenga uzalendo wa kweli,ukiamua kufuta chai ofisini kwenu na hela zote kununulia madawati shule zote za tanzania ambazo gharama yake ni chini ya bilion 150 utakuwa mzalendo,ukisema kuanzia leo ukikamatwa na rushwa kubwa au ndogo  unapata adhabu kali utakuwa mzalendo,ukiwataja wauza unga na wale waliokwpua hela za epa na kurudisha kimya kimya utakuwa mzalendo,ukisema wabunge wako wajadli maoni ya wananchi waliowatuma bungeni utakuwa mzalendo..
         Lakini kualikwa kuzindua uzalendo wa kinafiki si sawa,maana hata hao walioandaa tamasha hilo si wazalendo kwa matendo yao,na hao wasanii waliojinasibu hapo si wazalendo hata kidogo,baadhi yao wanajihusisha na biashara haram ya madawa ya kulevya na uchafu mwingi tu ambao hauna undungu na kitu kiitwacho uzalendo.

 Mh  rais  naamni umekuwa ukisafiri sana katika mataifa ya wenzako na kujionea mengi,ni jambo jema kusafiri na kuona mengi lengo likiwa ni kujifunza na kujifunza ni chakula cha ubongo wowote ulio hai,huko unakokwenda kweli umeona uzalendo unahubiliwa katika vyombo vya habari na huku serikali zao zikinuka rushwa na kutokutenda matakwa ya watawaliwa?naamini uwezo wako wa kusikiliza watu ni mkubwa na ni jambo jema,lakini pamoja na hayo yote naamni haukuwa muda mwafaka wa wewe kwenda kuzindua kitu ambacho macho yake yanaona karibu kiasi hiki....

   Kuna wasanii ambao hata tungo zao hazisemi kwamba wao ni wazalendo,ila wako hapo kuhakikisha masilahi yao yanapatikana na pia kuwa karibu na watawala katika bara letu la afrika kunasaidia watu kufanya maovu yao kwa maana wanao watu wa kuwalinda ..

 POLENI SANA DUNIA INAKWENDA KASI KAMA UPEPO NA AKILI ZINAKUA KILA UCHWAO---SIKU ZOTE MTU HURU NI YULE MWENYE MAWAZO HURU





         

HUYU NDIYE ANAYE KUTESA NA HOFU YA UKIMWI---DR ROBART GALLO

Habari,
     katika dunia ya leo kila mmoja wetu huenda amepata madhara ya moja kwa moja au kwa ndugu na jamaa  zake kuhusu tatizo hili la ugonjwa wa ukimwi ambalo kuna binadamu mwenzetu alitengeneza,

     Mnamo 1971 nchini marekani kuna daktari mmoja anayetambulikana kwa jina la Robert gallo aliandika kitu kinachoitwa (1971 special virus paper)kwenda kwa  U.S SPECIAL VIRUS PROGRAM hiki ni kitengo maalum katika serikali ya marekani.baada ya kupeleka andiko lake katika serikali yake,serikali ilikubali kudhamini mradi huo,na kama ulikuwa hutambui tambua leo marekani hawezi kudhamini kitu ambacho hakina masilahi kwake.
  
     Lengo la mradi huo ilikuwa na kupunguza ongezeko la watu duniani hasa watu weusi,na lengo lao ilikuwa katika bara la Afrika na Manhatan huko huko kwao marekani ambako kuna idadi kubwa ya watu weusi kwa nyakati hizo.

 Na hatimaye 1984 bwana Robert gallo akatangaza rasmi kazi yake ya maabara iliyodumu kwa takribani miaka 3 na hatimaye kikatokea kitu kinachoitwa H.I.V.

   Tangu hapo mpaka leo gonjwa hili la kutengenezwa limeua idadi kubwa sana ya raia wasio na hatia,bado lengo lao halijakamilka, likikamilika watajua cha kufanya tena, ni mtu huyu mmoja ndiye anayejenga hofu kwa watu bilion saba na kweli jaribio lake limeshinda kututia hofu na kutoa roho zetu.

    Kama binadamu hutakiwi kukata tamaa,kila siku lazima ujifunze na uwe tayari kufanya mabadiliko katika maisha yako,hiv ipo inaua watu na ukishindwa kuwa makini na maisha yako na wewe pia utakufa kwa mateso makubwa sana.tunao wasomi hapa kwetu ambao hata uwezo wa kupambanua mambo kisayansi hawawezi na kila siku tunaletewa dawa na majibu ya matatizo yetu na watu wale wale ambao tatizo lenyewe wamelitengeneza wao kwa faida zao.
            Baadala ya kuwa wapokeaji tu lazima tuwe na uwezo wa kuhoji haya mambo kisayansi,kupata ukimwi au kuteketea na janga hili kunatokana na TABIA,tabia zetu za kupuuza na kutopenda kuhoji mambo ndiko kunapelekea ndugu zetu kuangamia.....KAMA WEWE NI MSOMI HASWA,BASI BADILISHA DUNIA KWA FANI YAKO
DR.ROBERT GALLO


muda ni sasa  jenga taifa lako
DR. ROBART GALLO

NEW WORLD ORDER''' INAKULAZIMU UPATA UNDANI WAKE BILA CHEMBE YA HOFU

16 JUNE 2014,

       Habari yako ndugu msomaji wa blog hii,natumaini uu mzima wa afya njema na mungu wangu akubariki sana kwa kuamua kusoma habari hii,

       Hii si habari ngeni sana katika masikio yako na kama ni habari ngeni ,basi vuta pumzi na ujiweke tayari kiakili ili ubongo wako upate chakula,new world order huu ni mpango kabambe wa kuhakikisha dunia inakuwa moja kwa matakwa yao wenye mpango wao,kwa hiyo mabadiliko yote haya unayoyaona katika sayansi na jamii ni ukamilifu wa mpango huo.

      Haya si maoni ya dini fulani la hasha bali ni mpango kazi unaotekelezwa na watawala wa dunia wenye nguvu bila hata jamii yenyewe kujua kwa kina mantiki ya mpango huo,lengo langu ni kutaka kukuhimiza kwamba haya si majira ya kupuuza mambo ni majira ya hatari sana ambayo yanakulazimisha kujua kila nukta ya maendeleo ya dunia hii,maana tulipofika ukiacha mbali mafundisho ya imani zetu lakini hata wanasayansi na watawla wa dunia hii wanakiri kwamba dunia si mahala salama kwa maisha ya binadamu tena.

     NEW WORLD ORDER---kwa akili zao, wameweka mpango huu ambao unatekelezwa kwa ghalama yoyote ili kuwaaminisha wanadunia kwamba wao ndiyo wanayo majibu ya matatizo ya dunia hii,ambapo si sahihi.dhana hii imeanza kukubaliwa na watawala wetu,wanajamii wetu bila kujua madhara yake ni yapi baada ya kitambo kidogo,maana daima hakuna mpango wa binadamu uliosahihi kinyume na mungu muumba wa mbingu na nchi,
        JIULIZE

      Kwa nini kuna atm card,digital,umoja wa ulaya,vita za wakati wote,mashinikizo ya kishoga ,na mengine mengi,,,,LENGO LAO NI KUUNDA DUNIA MPYA WAITAKAYO,uwezo wa kupambana kimwili huna ila soma ili ujue kinachoendelea duniani
PICHA  NO 1

HIVI DIVYO DUNIA ITAKAVYOKUWA

Sunday, June 8, 2014

HII YA WABUNGE KUONDOLEWA KINGA YA KUSHITAKIWA NI USHINDI KWA WANACHI

Habari,
        Hizi siku mbili ni siku ambazo katika idara ya kusimamia na kutafsiri sheria MAHAKAMA imewatendea haki  watanzania baada ya haki yao kufichwa kwa miaka mingi katika mwavuli unaoitwa ubunge..
   Kwa sasa mbunge yoyote atakayoyasema bungeni kama ni ya kutunga au kuudhi kama yule mbunge wa ccm alivyotukana basi atashitakiwa kama raia mwingine wa kawaida,hili ni jambo ambalo linatia nguvu kwa wanaharakati kuendelea kudai haki nyingine zinazokandamiza uhuru wa mtu.
   Kwanza inatia kinyaa na ni aibu kwa mbunge tena kiongozi wa jamii anapiga picha cha ngono,zinazokiuka maadili ya taifa na madili ya uongozi,na bado kanuni zao zinabki kimya,hii haikubaliki kabisa,mimi naomba hawa wabunge wawili wote wa ccm wafukuzwe ubunge na nyadhifa zao nyingine maana hawafai na hawana tofauti na wahuni wa mtaani.
  Nitamshangaa sana rais wetu na spika wa bunge wakikaa kimya huku wabunge hawa wanadhalilisha taifa.na pia mahakama itupe mongozo tena,je hawa wabunge mtu mmoja mmoja anaweza kuwashitaki?mtwambie sheria inasemaje,
       Hili ni bunge la ajabu kabisa dunia halijawahi kutokea,na muda wenu umekaribia,
BUNGE LA TANZANIA 2014